Burudani

Gadna G Habash ajiengua Clouds FM

 

Mtangazaji wa Radio Clouds Fm Gardner G Habash Leo asubuhi majira ya saa mbili ametangaza rasmi kupumzika kufanya kazi chini ya Radio hiyo kwa muda usiojulikana.

Meneja vipidi vya Radio hiyo bwana Sebastian Maganga ambaye anasimama kama mwenyekiti wa mchakato huo alitangaza rasmi hatua hiyo ya Gardner pamoja na kumuweka live mtangazaji huyo aliyekuwa anatangaza kipindi cha Jahazi kilichojizolea umaarufu mwingi tangu kilipoanza kusikika miaka mitatu iliyopita.

Mtangazaji huyo amvaye pia ni mume wa Mwanamuziki Nguli nchini hapa, Lady Jay Dee, alisema ameamua kupumzika kwa hiari yake hivyo anaomba awekwe kando katika mchakato wa Novemba Noma unaoratibu shughuli nzima ya maoni kutoka kwa wadau wapenzi na wasikilizaji wa vipindi vya Redio hiyo.

Aidha katika siku ya Jumatatu ya wiki hii mtangazaji mwingine Sofia Kesi ambaye anatangaza katika kipindi cha Afrika Bambataa naye alitangaza kujitoa katika mchakato huo hivyo kufanya idadi ya watangazaji waliojitoa ama kupumzika kufanya kazi kuwa wawili mpaka sasa hivi.

Bongo5 itaendelea kufuatilia kwa karibu na kukupa matokeo ya mchakato huo ambao unatazamiwa kufika mwisho kesho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents