Bongo Movie

Gabo Zigamba adai yeye ni mkali wa kuigiza zaidi ya Ray Kigosi

Msanii wa filamu Gabo Zigamba, amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mkali wa kuigiza kumshinda mkongwe Ray Kigosi.
Gabo

Akizungumza katika kipindi cha ENewz cha East Africa Television, Gambo Zigamba amesema wasanii wapya wamekuja kuleta changamoto kwa wasanii wakongwe.

“Ray ana flavor (ladha) zake na wapo watu wapo wanampenda Ray lakini kuna watu zaidi ya Ray wanaweza kufanya vizuri zaidi ya Ray, ila naweza kusema mimi ni zaidi ya Ray kwani naweza kufanya kitu zaidi ya Ray, Ray akabaki amefanya na mimi nikafanya zaidi yake na watu wakapenda zaidi. Mimi siogopi mtu japo ukweli utabaki pale pale kuwa baba ni baba ila mtoto anaweza kufanya jambo vizuri hata zaidi ya baba yake,” alijigamba Zigamba.

Gabo kwa sasa anafanya vizuri sokoni na filamu yake iitwayo ‘Safari ya Gwaru’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents