Bongo Movie

Gabo awaka baada ya mtandao mmoja wa Kenya kudai yeye ni muigizaji wa nchi hiyo

Muigizaji anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu, Gabo Zigamba ameujia juu mtandao mmoja wa Kenya ambao umedai kuwa yeye ni raia wa Kenya.

Mtandao huo uliandika stori yenye kichwa cha habari “Gabo Kenyan-talented movie actor” .

Hata hivyo Ijumaa hii mtandao huyo uliamua kurekesha habari hiyo.


Jinsi kichwa cha habari hiyo kilivyokuwa kabla ya kubadilishwa

Muigizaji huyo baada ya kuona taarifa hiyo, kupitia instagram aliandika:

Kinachoweza kuondoa makucha haya ya majirani ni film tuu. Film is the best method of propaganda spreading. Na ili tufikie hapo ni kufanya kazi zenye ubora wa kidunia ili ziende duniani kufikisha ujumbe.. bado tuna deni kubwa la kuwavua nguo hawa wadhalimu.. hii vita ya nyenyenye za jirani viongozi wengi wana nafasi ya kuishiriki ila sioni ushirika wao. Nna hofu hata tukianza kutengeneza films za kuuambia ulimwengu juu ya machache yanayotangazwa na majirani mmh zisijeishia studio kisa ujirani mwema.. hio ni hofu yangu tuu.. kama trump anamuongelea Puttin on media vipi viongozi wa serikali yetu hawayaoni haya yote..? Mimi naamini serikali yetu inauwezo wa kuita press na media house za dunia na kuorodhesha yote yaliyodaiwa na wakenya kuwa yao na kuipa ujumbe serikali ya kenya . Mfano.. Tunajua mengi yatadaiwa kuwa ni raia tu binafsi na taasisi ndio zinajitamkia haya mambo. Yaani si kenyan government.
Lakini mimi najiuliz raia anapoongelea vitu kama Olduvai gorge ipo kenya mimi najiuliza darasani somo la historia kenya wanafundisha nini?
bado najiuliza wakenya wanafundishwa georaphia ya wapi mpaka waseme kilimanjaro iko kwao?
Mrisho mpoto miaka michache ilopita huko ughaibuni alishikishwa bendera ya kenya na wakenya,akaishusha bendera stegini. Hongera kwako mjomba. Sikupoteza nguvu zangu wakati wa kutoa mchango wangu kwako mjomba.. Ukitaka kuusimamisha moto nenda kwenye chanzo.. haya mambo ni ya history na geographia yaani namaanisha hutokana na elimu wanayopewa.. sasa swali ni kwamba kama oldivai na kilimanjaro ni viko kwao unashangaa nn wakisema Gabo ni wao au mpaka waseme Arusha nayo ni ya kwao????

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents