Burudani

G-Nako akana kumfahamu rapper Flowking Stone

G-Nako ameendelea kupinga tuhuma za kukopi wimbo ‘Go Low’ alioimba na Jux lakini pia amedai hakuwa anamfahamu rapper Flowking Stone kutoka Ghana mwenye wimbo wenye jina hilo na unaofanana na wake.

Wiki iliyopita kupitia kipindi cha Zero Planet cha Ice Fm, rapper huyo kutoka kundi la Weusi alikana kunakiri wimbo huo. Akiongea na kipindi cha E-News cha EATV, G-Nako amesisitiza kuwa hakugeza wimbo huo wala hajawahi kumsikia huyo msanii hapo mwanzo.

“Mimi sijawahi kusikia hii nyimbo ‘before’ wala kumsikia huyu msanii ‘to be honest’ na siku zote mimi siamini katika ku-copy kazi ya msanii mwingine kwa sababu naamini kabisa siwezi kupata njia yangu mimi kama ninaweza kumkopi msanii mwingine,” amesema rapper huyo.

Wimbo wa Go Low wa FlowKing Stone umetoka Agosti 9 mwaka jana wakati huo huo wimbo wa G Nako umetoka mwezi uliopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents