Burudani

Future na Ciara wafikia makubaliano ya namna ya kumlea mtoto wao

Future na Ciara wamedaiwa kufikia makubaliano ya njia nzuri ya kumlea mtoto wao wa kiume mwenye miaka 2, Future Zahir Wilburn.

Tovuti ya TMZ imeripoti kuwa wapenzi hao wa zamani wamekubaliana kumlea pamoja mtoto wao, japo mtoto huyo atakuwa na mama yake muda mwingi.

Mapema mwezi huu, Ciara aliifuta kesi ya kuchafuliwa dhidi ya Future aliyeshutumiwa kukosoa uhusiano wake na mchezaji wa NFL, Russell Wilson ili kuzipa kiki ngoma zake.

Russell na Ciara wanatarajia kupata mtoto wa kwanza hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents