Burudani

Fundi Samweli kutayarisha wimbo wa Marco Chali, ni sehemu ya mradi wake kama msanii

Producer wa Sweden, Fundi Samweli, atatayarisha wimbo mpya wa producer wa MJ Records, Marco Chali.

ffd9f940961b11e39166126eed24a06d_8
Fundi Samwel akiwa na Marco Chali kwenye studio za MJ Records

Marco ameaimbia Bongo5 kuwa Fundi Samweli ni mtayarishaji wa muziki anayemkubali na anaupenda muziki na hivyo kufanya naye kazi itakuwa ni kitu kizuri kwake. Amesema wamezungumza na producer huyo kuwa atamtengenezea beat ambayo Marco ataiandikia na kurekodi sauti kwenye studio ya MJ ambazo atamtumia Sweden ili azioanishe na beat yake na kukamilisha kila kitu.

Marco amesema wimbo atakaofanya na Fundi Samwel utakuwa sehemu ya mradi anaoufanya yeye kama msanii na maproducer wengine wakubwa wa Tanzania na kwamba yeye hatoshiriki katika kutayarisha chochote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents