Burudani

French Montana akiri anataka kutumia umaarufu wa mpenzi wake Khloe Kardashian kwa faida

Miongoni mwa couple za watu maarufu duniani, wapo ambao huingia kwenye uhusiano kwasababu ya mapenzi ya kweli, wapo ambao huwa pamoja kwa sababu za kibiashara kutokana na umaarufu wao, na wengine huingia mapenzini kwa sababu zote mbili.

Khloe-Kardashian-Dating-French-Montana

Rapper French Montana ambaye ana’date’ na mdogo wa mke wa Kanye West, Kim Kardashian aitwaye Khloe Kardashian, amesema yeye anautumia vizuri umaarufu wa mpenzi wake kwa faida.

Montana amefanya mahojiano na jarida la Billboard, na kukiri kuwa hana tatizo na ‘attention’ ya ziada anayoipata kutokana na kuwa na uhusiano na Khloe Kardashian wa reality show maarufu ya familia ya mpenzi wake ‘Keeping Up With The Kardashians’ (KUWTK), sababu inamuongezea fanbase.

french

“I want to capitalize on it(umaarufu wa Khloe), I’ll get a fan base from everywhere. I just hope I’ll be able to connect with everything that’s going on.” Alisema.

Montana mwenye miaka 29 na Khloe mwenye miaka 30 walithibitisha uhusiano wao mwezi Julai katika mahojiano yao ya kwanza kama couple na Angie Martinez wa Power 105.

Khloe pia ametokea kwenye video mpya ya boyfriend wake inayoitwa ‘Don’t Panic’, kitu ambacho kitasaidia kuiboost video hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents