Burudani

Fox yawaomba radhi Wakenya kwa kutumia video ya shambulio la kigaidi la Westgate Mall kwenye series ya 24 Legacy

Fox Network imewaomba radhi Wakenya baada ya kurusha video ya ukweli ya shambulio la kigaidi la Westgate Mall na kuiweka kwenye series yake mpya, 24 Legacy.

Msemaji wa kituo hicho, Chris Alexander alisema waandaji wa show hiyo wanajutia kutumia tukio hilo kwenye mkasa wa kutunga. Waandaji wa show hiyo wamedai kuwa video hiyo itaondolewa.

“In episode 4 of 24: Legacy we regretfully included news footage of an attack in Nairobi. It will be removed from all future broadcasts and versions of the show. We apologise for any pain caused to the victims and their families and are deeply sorry,” yalisema maelezo toka kwa waandaji wakuu, Evan Katz na Manny Coto.

Wakenya walichukizwa vikali kutokana na kitendo hicho cha kutumia video za shambulio hilo la miaka mitatu iliyopita lililosababisha vifo na taharuki kubwa. Kama kawaida ya Wakenya, walitumia Twittter kuishambulia Fox kwa hashtag, #SomeoneTellFox kulaani kitendo hicho.

Kwenye episode hiyo, shambulio hilo limeandikwa limetokea Alexandria, Misri ambapo watu 200 waliuawa. Katika shambulio la Westgate Mall September 21, 2013, watu 67 waliuawa na wengine 175 kujeruhiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents