Burudani

Forbes yatoa orodha ya wasanii 5 wa Hip Hop matajiri zaidi 2014, Diddy awashinda Jay Z, Dre na 50 Cent

Forbes imetoa orodha ya wasanii wasanii watano wa Hip Hop matajiri zaidi 2014. Sean “Diddy” Combs , zamani Puff Daddy au P Diddy na sasa Diddy ndiye anayeongoza katika orodha hiyo kwa kuwa msanii tajiri zaidi wa Hip Hop 2014 kwa mujibu wa Forbes.

Forbes-Wealthiest-Hip-Hop-Artists-April-2014

Utajiri wa Diddy unakadiriwa kuwa dola milioni 700, ikiwa imeongezeka dola milioni 120 kutoka mwaka jana huku vyanzo vya utajiri wake vikitajwa kuwa ni Revolt TV/Diageo’s Ciroc.

Anayefuatia katika nafasi ya pili ni producer Andre Young aka Dr. Dre ambaye ana utajiri unaofikia dola milioni 550. Utajiri wake umetokana na mauzo ya headphones za Beats by Dr. Dre.

Nafasi ya tatu imeshikwa na Shawan Carter aka Jay Z, kwa utajiri wa dola milioni 520 huku vyanzo vya utajiri huo vikitajwa kuwa Rocawear Sale/Live Nation/Roc Nation.

Nafasi ya nne imekamatwa na Bryan Williams aka Birdman, huku utajiri wake ukitokana na Cash Money/YMCMB/GT Vodka.

Wa mwisho katika orodha hiyo aliyeshika nafasi ya tano ni Curtis Jackson aka 50 Cent, mwenye utajiri wa dola miliono 140, vyanzo vyake vikitajwa kuwa ni Vitamin Water/SMS Audio/SK Energy.

Story hii ni sehemu ya story itakayotoka katika jarida la Forbes la May 5.

The Forbes Five: Hip-Hop’s Wealthiest Artists 2014

1.Sean “Diddy” Combs | $700 Million | Revolt TV/Diageo’s Ciroc
2.Andre “Dr. Dre” Young” | $550 Million | Beats by Dr. Dre Headphones
3.Shawn “Jay Z” Carter | $ 520 Million | Rocawear Sale/Live Nation/Roc Nation
4.Bryan “Birdman” Williams | Cash Money/YMCMB/GT Vodka
5.Story kamili ya orodha hii itatoka katika toleo la May la jarida la Forbes.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents