Habari

Forbes 2017: Mohammed Dewji aongoza orodha ya matajiri vijana Afrika

By  | 

Tovuti ya Forbes imemtangaza Mkurugenzi wa kampuni ya METL, Mohammed Dewji kuongoza orodha ya matajiri vijana kwa Afrika akiwa na umri wa miaka 41.

Utajiri wa Dewji umetajwa kuwa ni dola bilioni 1.4. Wakati huo huo ametajwa kushika nafasi ya 16 kwenye orodha ya matajiri wote Afrika huku Aliko Dangote wa Nigeria akiendelea kukalia kiti hicho akiwa na utajiri wa $12.1 bilioni.

Kwa upande wa wanawake mtoto wa Rais wa Angola, Isabel dos Santos anaongoza kwa kuwa na utajiri wa $3.2 bilioni akifuatiwa na Folorunsho Alakija wa Nigeria mwenye utajiri wa $1.6 bilioni.

Bonyeza hapa kutazama orodha hizo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments