Burudani

Flaviana Matata na Gado watajwa miongoni mwa Waafrika wenye ushawishi 2014

Mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata na mchoraji mahiri wa vibonzo anayefanyia kazi nchini Kenya, Godfrey ‘Gado’ Mwampembwa, wametajwa na jarida la New Africa kwenye orodha ya mwaka 2014 ya Waafrika wenye ushawishi zaidi.

10665830_531746743623030_898097850455292967_n

Flaviana ameungana na muigizaji wa Kenya, Lupita Nyong’o kwenye orodha hiyo yenye wanawake 40.

Hata hivyo Nigeria na Afrika Kusini ndizo zimetawala orodha hiyo zikiwa na watu 33 na 27.

Kwenye orodha hiyo pia kuna viongozi wanne wa nchini wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta, Rais al-Sisi wa Misri, Rais Déby wa Chad na Museveni wa Uganda.

Soma zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents