Burudani

Flaviana Matata aushtaki mfuko wa PSPF mahakamani

Mwanamitindo wa Tanzania anayefanya kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata ameushitaki mfuko wa pensheni wa PSPF mahakamani akitaka alipwe shilingi milioni 165 kutokana na mfuko kwa kosa la kukiuka mkataba wao kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania.

Flaviana

Flaviana ambaye ni balozi wa mfuko huo wa PSPF kupitia kwa mwanasheria wake Edward Lisso wa Law Associates Advocates wameushitaki mfuko huo kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha inadaiwa kuwa Mwanamitindo huyo ameiomba mahakama iuamuru mfuko huo kumlipa kiasi cha milioni 100 ikiwa ni kama fidia kutokana na kupoteza muda na fedha nyingi ikiwa ni pamoja na kukosa fursa nyingine za kibiashara na makampuni mengine wakati akifanya mawasiliano na mlalamikiwa na ugumu alioupata wakati akifuatilia suala hilo.

Mwanamitindo huyo ameongeza kuwa anakula hasara ya kiuchumi kwa vile picha zake zinaendelea kutumika kinyume na mkataba wake na mfuko huo. Shauri hilo lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Magreth Bankika na litatajwa Septemba 22, mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents