Bongo Movie

Filamu ya Tanzania ‘Dogo Masai’ kuwania tuzo nchini Marekani

Filamu ya Kitanzania iitwayo ‘Dogo Masai’, imetajwa kuwania tuzo za Silicon Valley African Film Festival (SVAFF) za nchini Marekani. Filamu hiyo imetayarishwa na kuongozwa Timoth Conrad Kachumia, wa Timamu African Media.

Dogo Masai imeingia kwenye kipengele cha Best Feature Film ambapo inashindana na filamu kutoka katika nchi mbalimbali zikiwemo Afrika Kusini, Malawi, Misri, Nigeria, pamoja na Uganda.

“Kutoka nchini Tanzania Dogo Masai ni filamu pekee ambayo imeingia kwenye mashindano hayo, lakini kwa East Africa ni filamu mbili ambayo moja ni kutoka Uganda na hapa kwetu,” amesema Timoth.

Kuona list nzima ya filamu zilizochaguliwa kushindana na DOGO MASAI bofya hapa.

Licha ya kufanikiwa kuingia kwenye tuzo hizo za Marekani, filamu hiyo imechaguiwa kuingia kwenye tamasha la Rome Independent Film Festival (RIFF) la nchini Italia.

Ingia hapa kuona.

Si mara ya kwanza kwa Timoth kuandaa filamu ikaingia kwenye tuzo kubwa barani Ulaya. Mwaka mwaka jana Timoth Conrad alihusika katika kuandaa filamu iliyoitwa Mdundiko iliyoongozwa na Jackson Kabirigi. Nayo ilileta heshima nchini baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo hizo za SVAFF ambazo zinaandaliwa nchini Marekani. Licha ya kunyakua tuzo hizo lakini pia ni filamu ambayo ilipata nafasi ya kuchaguliwa kushindana kwenye tuzo nyingi barani Africa na kwingineko.

DOGO MASAI ni filamu ya kitanzania inayomuelezea kijana Dogo masai ambaye anaamua kuuvaa uhusika wa kuwa muonekano wa kimasai baada ya kufanyiwa vitendo vya kinyama na mjomba wake. Hivyo anaingia katika safari ndefu ya kutafuta suluhisho la yote aliyofanyiwa. Ni filamu ya kusisimua na kuhuzunisha pia kutokana na ugumu wa maisha anaokutana nao Dogo Masai.

Wahusika kwenye filamu hiyo ni pamoja na Omary Clayton, Hissani Muya, Mainda Suka, Julieth Samson na Mukasa Tabani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents