Bongo Movie

Filamu ya ‘Chausiku’ yampa deal Shamsa Ford nchini Kenya, azungumzia anavyojiweka mbali na skendo

Msanii wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford anayetamba na filamu kama ‘Chausiku’ na ‘Bado Natafuta’, amezungumzia jinsi filamu ya ‘Chausiku’ inavyoendelea kumpa deal mbalimbali.

chausiku

Akizungumza na Bongo5 leo, Shamsa amesema filamu ya ‘Chausiku’ inaendelea kumpa deal kubwa kutoka kwa makampuni pamoja na heshima kwa jamii kutokana na kazi zake kuwa nzuri.

“Chausiku stori niliandika mimi mwenyewe na ndiyo maana imekuwa filamu kubwa, siyo hiyo tu filamu zangu zote ninazo fanya zinafanya vizuri sokoni. Kuna kampuni ya Kenya imeniambia inanihitaji kuna kazi, kwa sasa siwezi kuizungumzia zaidi kwa sababu bado kuna mambo hayajakamilika, pia walisema kuna msanii mkubwa wa nje na yeye atakuwa kwenye hiyo kazi,” alisema Shamsa.

Pia Shamsa alitoa sababu za kutopenda skendo kama wasanii wengine ambapo amedai kuwa anatambua nini kimempeleka kwenye filamu.

“Kwanza nina mtoto sitaki aje baadae asikie mama yako alikuwa hivi na hivi, pia ni mke wa mtu kwahiyo najitambua halafu kabla sijaingia kwenye filamu mama yangu alinipinga sana, mimi nikamwambia mama mimi naenda kufanya kazi iliyonipeleka na siyo kazi nyingine, kwaiyo akaniruhusu mpaka sasa hivi mama yangu anafurahia na anajua nini nafanya. Kwahiyo maswala ya kusema sijui nifanye tukio fulani ili niwe juu hapa hakuna mimi ni kazi tu ndo itaniweka juu,” alisema Shamsa.

Katika hatua nyingine Shamsa alizungumzia wadada wa filamu wanaoichafua tasinia ya filamu kwa skendo za ajabu ambazo amedai zinawashushia heshima.

“Sisi ni kioo cha jamii, tunatakiwa kufanya vitu ambavyo hata watoto wetu baadae wakae na wenzao na kuzungumzia mazuri ya wazazi wao, sasa ukiwa na mambo mengi ya ajabu utakuja kuwapa shida watoto wetu, sina kikubwa cha kusema nataka tujiheshimu wenyewe na tushirikiane,” alimalizia Shamsa Ford.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents