Michezo

Fifa ya mfungia maisha refa wa Ghana

Refa ambaye ni raia wa Ghana Joseph Lamptey, amefungiwa maisha na shirikisho la kandanda Duniani Fifa, baada ya masuali kuibuka jinsi alivyosimamia mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Senegal na Afrika Kusini Novemba 2016, iliyopita.


Joseph Lamptey

Afrika Kusini ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1 lakini Senegal ikalalamika kwa shirikisho la Fifa.

Walisema kuwa Lamptey aliwapa Afrika kusini penalti licha ya naibu refa kuashiria kuwa ingekuwa kona.

Wengi waliuliza maswali kuhusu kona hiyo wakati huo, kikiwemo kitengo cha michezo cha BBC kilichoripoti kuwa Afrika Kusini iliongoza baada ya panelti hiyo yenye utata.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents