BurudaniHabari

Fiesta yaanzia Billicanas

Fiesta 2006UFUNGUZI wa tamasha kubwa la muziki linalofanyika kwa mwaka mara moja linalojulikana kama ‘FIESTA’ lilizinduliwa juzi kwenye Ukumbi unaotamba Afrika Mashariki na Kati, Club Billicanas, jijini Dar es Salaam.

Fiesta 2006Na Victor Masangu

UFUNGUZI wa tamasha kubwa la muziki linalofanyika kwa mwaka mara moja linalojulikana kama ‘FIESTA’ lilizinduliwa juzi kwenye Ukumbi unaotamba Afrika Mashariki na Kati, Club Billicanas, jijini Dar es Salaam.

Katika ufunguzi huo ambao ulihudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki kutoka sehemu mbali mbali ulikuwa ni moto wa kuotea mbali kutokana na kupata buruduni ya kutosha iliyokuwa ikiporomoshwa na baadhi ya wasanii.

Ufunguzi huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwatambulisha baadhi ya wasanii wa kizazi kipya wanaotarajiwa kufanya vitu vyao siku ya tamasha hilo Julai 29, mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa ni burudani tosha kwa wakazi wa Dar es Salaam waliopata bahati ya kushuhudia wasanii mbali mbali wakipanda jukwaani kwa nyakati tofauti na kuanza kutoa burudani.

Wa kwanza alikuwa ni msanii Jo- Makini, aliyetoa burudani ya kutosha kwa mashabiki, ndipo baada ya hapo kundi zima linalotamba nchini Kenya la Necessary Noise walifanya vitu vya uhakika na kuzikonga nyoyo za mashabiki.

Mbali ya hao pia burudani iliendelea, kushika kasi kadiri ya muda ulivyokuwa unakwenda pale alipopanda Banana Ally Zoro na kundi lake la kucheza, pia baada ya hapo alipanda msanii Mb Doggy kutumbuiza na wimbo wake wa Latipha.

Burudani ilizidi kuwapagawisha mashabiki pale mwanadada mahiri Rehema Chalamila ‘Ray’ alipojitokeza jukwani na kuanza kumwaga uhondo wa burudani wa aina yake, na msanii mwingine kutoka kundi la East Coast Team Crazy Gk alivamia jukwaa na kuimba wimbo wa ‘Itikadi Zetu’.

Shangwe na mlipuko wa mayowe yalikuja pale ulipowadia muda wa kumtambulisha Dj maarufu wa kituo cha Televisheni ya Channel ‘O’ alipokamata mashine na kuanza kuonyesha umahiri wake katika kucheza nyimbo na kuwadatisha mashabiki pale alipoanza kusugua kwa kutumia mguu, kichwa, kofia, shavu pamoja na ulimi.

 

Source: TanzaniaDaima

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents