Bongo5 Makala

Fiesta Dar: Yaliyojiri, mbwembe, vituko na tuliyojifunza

Show ya Serengeti Fiesta 2014 jijini Dar es Salaam imeingia kwenye historia ya kuwa matukio makubwa ya burudani yaliyozungumzwa zaidi kwenye mtandao wa kijamii mwaka huu baada ya tuzo za KTMA 2014.

page

Maelfu ya tweets kupitia hashtag ya #SerengetiFiesta2014 yaliifanya show hiyo kutrend duniani kote. Show hiyo ilitoa picha halisi ya namna muziki wa Tanzania ulivyo na nguvu barani Afrika na kwamba huenda Fiesta ni tukio kubwa zaidi la kiburudani barani Afrika.

“Imani yangu imepata nguvu sana jana,kuwa wabongo wanapenda mno wasanii wao(na mziki wao)..sana,sana…luv za kupitiliza,” aliandika Mwana FA.

“Fundisho tu kuwa hakuna sababu ya kuendelea kubabaikia mziki wa nje(HASA WA KIPOPO)..kwy market hii watu wetu wakipewa nguvu tu wanakinukisha na wanadeliver,hakuna cha wapopo wala ‘wanyamwezi’..tia mkwanja mrefu watu wetu,hakikisha mzunguko wa hela unabaki bongo,tutabeba mziki na uchumi wetu kwa wakati mmoja,ndege kibao jiwe moja.. noma sana.”

Ujio wa T.I., rapper anayejulikana kama mfalme wa Kusini, nchini Marekani, ni uthibitisho tosha kuwa waandaji na wadhamini wa tamasha hilo wamefika mbali. Iliwachukua miaka mitatu ya kumtafuta rapper huyo hadi kufanikiwa kumpata mwaka huu. T.I. amekuja Tanzania katika kipindi ambacho yupo hot duniani kote kutokana na ujio wa album yake ‘Paper Work’ inayotoka Jumanne hii, October 21.

T.I. na wasanii wengine wa nje wakiwemo Davido, Waje, Patoranking, Victoria Kimani na wasanii wa ndani, walifanikiwa kuvuta umati wa kihistoria unaodaiwa kufikia watu 50,000!

Mwandishi wa Bongo5, Yasin Ng’itu ambaye alikuwa shuhuda wa show hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho na kuweza kuchukua picha zote ulizoziona kwenye website hii, anatuelezea namna mambo yalivyokuwa.

Kusema kweli show ya Fiesta mwaka 2014 ilikuwa nzuri kutokana na mpangilio wa show kwa wasanii, mavazi pamoja na kuwepo kwa ratiba nzuri ambayo iliifanya show hiyo isichoshe wala kuboa wadau waliokuja kuburudika.
Kubwa na jipya lililojitokeza kwenye show hiyo ni jinsi screen kubwa iliyokuwa imefungwa kwenye jukwaa iliyokuwa ikitumika kuwaonesha mashabiki wa muziki kujua nini kunakuja.

Pamoja na hivyo, watu walipata fursa ya kuangalia kwa mara ya kwanza video ya mpya ya wimbo wa Mwana FA ‘Mfalme’ ambayo bado haijatoka rasmi.
Show ya Fiesta ilianza mapema saa 12 jioni huku wapenzi wa muziki wa Dar es Salaam walijitokeza mapema kabisa kuhakikisha hakuna kinachowapita.

Licha ya mashabiki kusubiria show ya mkali kutoa T.I., walisubiria kuona show za wasanii wao huku kila mmoja akisubiria show za wasanii wanaofananishwa na wapinzani wa jadi Simba na Yanga, Diamond Platnumz na Alikiba ambao kwa muda mrefu hawajawahi kupanda jukwaa moja. Tegemeo la mashabiki wao lilikuwa ni moja tu; kila mmoja amfunike mwenzie.

Pamoja na ligi ya wasanii hao wawili, wasanii wengine pia walifanya show kali na walionekana kujipanga. Ni kutokana na drama inayowazunguka Diamond na Alikiba ndio maana show zao zimekuwa habari ya mjini na kwa uhakika hicho kilikuwa hakiwezwi kuepukwa.

Ali-Kiba-2

Alikiba alikuwa wa kwanza kupanda kabla ya Diamond. Alipopanda mtoto huyo wa Kariakoo shangwe nyingi zilisikika. Mashabiki wake waliimba naye mwanzo mwisho.

Baada ya hapo alishuka na kumpa nafasi mdogo wake, Abdu Kiba na kuimba nyimbo kadhaa na kisha Ali kurejea tena akiwa akiwa mavazi mengine. Ilionekana kuwa burudani aliyotoa haikutosha kwakuwa mashabiki wake waliendelea kumtaka aendelee kuwasha moto japo ombi lao halikutimizwa.

Zamu ya Diamond ilifika. Aliwaacha hoi pale alipoonekana akiwa na gwanda za kijeshi. Kabla hata hajapanda jukwaani screen ya tamasha hilo ilianza kuonesha mwanajeshi ambaye alikuwa Diamond mwenyewe akiweka sawa silaha ili kujiandaa na pambano lake. Alipanda jukwaani na dancers zake wa siku zote ambao nao walikuwa na gwanda za JWTZ.

Diamond-alipanda-na-gwanda-za-jeshi (1)

Shangwe zake hazikuweza kudumu kwa muda mrefu na siwezi kujua sababu ila mashabiki wa muziki walianza kumzomea msanii huyo. Nashindwa kuamini kwamba watu hao walipangwa kufanya hivyo kama kambi ya Diamond ilivyodai
Hiyo ni kutokana na jinsi sauti zilivyokuwa zikisikika ambazo hazikuwa za kikundi kimoja. Ilionesha ni watu wengi walifanya hiyo. Hicho kilikuwa kitu kibaya kwake na ni wazi kilikata kabisa mood yake.

Zilisikika kelele nyingi kutoka uwanjani hapo zikisema ‘Kiba, Kiba, Kiba, Kiba’ kwa muda wa kama dakika tatu hivi wakati Diamond akitumbuiza.
Lakini baada ya kushuka kwa mara ya kwanza alipanda tena akiwa na Davido na kuimba wimbo wao ‘Number One’.

Baada ya drama zote hizo na wasanii wengine kutumbuiza, ndipo T.I. alipopanda kukamilisha kile kilichomtoa Atlanta, Georgia hadi Tanzania. Alianza kwa kuimba nyimbo za kitambo kidogo, Top Back na Rubberband Man ambazo watanzania wengi wanazifahamu. Pamoja na wakati mwingine kuonekana bado alikuwa na uchovu wa safari, energy aliyokuwa nayo Tip ilitosha kuuamsha uwanja na mara nyingi watu walisikika wakiimba naye.

T.I. pia aliamua kushow love kwa P-Square kwa kutumbuiza kidogo wimbo waliomshirikisha ‘Ejeajo’ lakini pia kuwapa shavu Nico na Vinz kwa kuchana mistari kwenye wimbo wao ‘Am I Wrong. Pamoja na hivyo nahisi T.I. alitakiwa kupewa maelekezo ya nyimbo gani ambazo Watanzania wangependa kumuona akiziimba. Kwa mfano wimbo kama ‘Blurred Lines’ ambao alishirikishwa na Robin Thicke ulifanya vizuri kwenye chart duniani lakini sio wimbo wenye taste Watanzania wanaweza kuipenda.

Wimbo kama ‘Fancy’ wa Iggy Azalea pia ambao aliuonjesha kidogo ni zile zile ambazo audience ya Kitanzania haziwezi kuzielewa. Kama ningepata fursa ya kumwambia nyimbo za kutumbuiza basi nyimbo kama Get Back Up, Got Your Back, Big Thangs Popping, I am Back, Yeah Ya Know (Takers), na zingine.

Kwa ujumla show ya Fiesta Dar mwaka huu imekamilika kwa kishindo kikuu ukilinganisha na ile ya mwaka uliopita ambapo kulikuwa na matatizo ya sauti na vyombo.

Fiesta inaipa sifa Tanzania na wengi wanatamani wangekuwa na tamasha kubwa kama hili, tujivunie.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents