Burudani

Fid Q kuachia documentary ya Bongo HipHop, itaelezea chimbuko lake

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, amesema anatarajia kuachia documentary itayoelezea historia ya hip hop ya Tanzania.

Fid q

Fid Q amesema documentary hiyo itaelezea muziki wa Hip Hop ulipotokam, ulipo na una[pokwenda.

“Ninafanya documentary ya bongo Hip Hop, itaelezea Hiphop ilipo ilikotoka na inapokwenda,” Fid ameiambia Bongo5. “Pia itaelezea maisha ya Watanzania kuanzia kwenye siasa, utamaduni na mambo mbalimbali ambayo yapo kwenye jamii ya wana Hip Hop. Itapambanua biashara ya muziki wa Hip Hop.”

Katika hatua nyingine, Fid Q amesema project anayosimamia kwa sasa ni ujio wa album kutoka kwa Vijana wa Ujamaa Hip Hop Darasa anaowasimamia.

“Kwanza project ambayo kwa sasa nipo nayo muda wote ni ya Ujamaa Hip Hop Darasa ambao tayari wametoa ngoma yao ya kwanza inaitwa Ujamaa,” amesema rapper huyo. “Sasa hivi wako mbioni kuachia ngoma ya pili, lakini pia katika ujamaa kuna watu ambao wako tayari kufanya album kwa mfano kuna Chikolo yupo tayari kufanya album ambaye ameshatoa wimbo wake wa kwanza unaitwa Mvua ya Mawe. Kuna mwingine anaitwa Nasri yupo tayari kufanya album, Kevi alikuwa tayari kufanya mixtape lakini ameenda shule India juzi na wengine. Kwahiyo hiyo ndio project inayonifanya niwe busy kidogo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents