Burudani

Fid Q azungumzia tofauti ya kufanya Hip Hop ngumu na laini na faida zake

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q ameelezea kwanini kuna baadhi ya wasanii wanafanya Hip Hop ngumu na wengine wakifanya laini.

Fid Q akiwa  na mchumba toka Geita

Fid ameiambia Bongo5 kuwa kila msanii anatakiwa kufanya kitu ambacho mashabiki wake wanapokea.

“Unajua mwisho wa siku watu tunafanya muziki na muziki ni Hip Hop. Kwahiyo kinachopendeza ni kwamba tunafanya kitu ambacho watu wetu wanakipokea haijalishi mtu anafanya laini au ngumu ilimradi ni Hip Hop,” amesema Fid. “Naomba ujue kitu kimoja, mimi nina heshima yangu na muziki unatakiwa uwe hivyo wote tukiwa maskini nani atamsaidia mwenzake au wote tukiwa matajiri nani atamtuma mwenzake? Kuna mgawanyiko na vitu kama hivyo. Mimi niko sawa ninachokifanya na sioni kama kuna tatizo, hakuna Hip Hop sana kuna Hip Hop ambayo inahitaji mtu kufikiria ili aelewe ujumbe ambao unakuwa umewekwa kule ndani. Kwahiyo cha msingi mtu akisema Hip Hop ngumu mimi huwa nasema hapana yeye ndo ana kichwa kigumu na kitu kigumu kufunguka ni akili iliyojifunga,” aliongeza Fid Q

Fid Q alidai kuwa kutunga mashairi ambayo yanaeleweka mapema kwenye nyimbo za Hip Hop ni vizuri ila kuwapa mashairi ya kufikirika ni vyema zaidi.

“Kuwapa mashabiki watu kitu ambacho watakielewa mapema ni vizuri ila kuwapa mashairi ya kufikirika ni vyema zaidi,” alidia Ngosha. “Kwa sababu tunasema kwamba, kizuri ni kizuri na chenye ubora ni bora, pia huwa tunasema ‘take time to think it’s a source of power’, tenga muda wa kufikiri kwa sababu huko ndo kuna vyanzo vya nguvu zote. Kwahiyo kama tutaweza kuwafanya wananchi waweze kufikiria kidogo itasababisha waweze kufikiria vyema na kwa kufikiria kwao vyema wataweza kusaidia jamiii kubwa ya watanzania. Sababu tunatokea Tanzania nchi ambayo inasumbuliwa na vitu vitatu ujinga, maradhi na umaskini. Kama tutaweza kufanikiwa kuondoa ujinga na maradhi, umaskini utaondoka wenyewe. Sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka na kila mtu yupo sawa anachokifanya cha msingi wote tunafanya Hip Hop ndio maana hata unasikia kuna wanajeshi wa anga, wa ardhi na wengine wengi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents