Burudani

Fid Q aeleza sababu ya kumtaja Wakazi na Nikki Mbishi kama wasanii wa kuangaliwa mwaka huu

Fid Q amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa juu ya rapper Wakazi na Nikki Mbishi kuwa ni wasanii wa kuangaliwa zaidi kwa mwaka huu.

Akiongea na Bongo5, Fid amesema, “Nilikuwa najaribu kumulikia mwanga juhudi zao ambazo wamekuwa wakizionyesha kwenye sanaa yao.”

“Kwa mfano mtu kama Wakazi kwa mwaka anaweza akawa na mixtape tatu na ndani yake kunaweza kukawa na ngoma kama nane nane. Wakati huo huo kuna wasanii kwa mwaka wanatoa ngoma moja lakini yupo kwenye mainstream na anafan base kubwa so wanasurvive,” ameongeza.

“Sanaa haihitaji hiyo kitu ila inahitaji variety kwahiyo hawa wamekuwa wakitupa variety, vitu tofauti tofauti kila siku. Kuna wakati bNikki Mbishi alikuwa anatoa ngoma kila wiki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents