Burudani

Fid Q adai aliwahi mno ujio wa album ya pamoja na Chidi Benz

Fareed Kubanda aka Fid Q anahisi aliwahi mno kutangaza ujio wa album yake ya pamoja na Chidi Benz.
Fid Q

Fid ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa wakiingia studio wanajitahidi kufanya ngoma mbili kwa mpigo ili kuharakisha project hiyo huku akidai pia katikati ya mwezi December wataachia wimbo wa kwanza.

“Tulichokesea sisi ni kuitangaza kwamba tunaifanya. Unajua mara nyingi, formula yangu especially mwaka unaokuja nimekuwa sipendelei kuongea kitu kabla sijakimaliza. Project tunaifanyia kazi. So far tunaenda kama track ya tatu mpaka sasa na tunatarajia kurelease moja yaani katikati ya December. Kwahiyo watu wakae tu mkao wa kula kwamba Fid Q na Chidi Benz wanakuja. Unajua tunachofanya mimi na Chidi mara nyingi tunaingia studio na tunafanya ngoma mbili kwa siku moja kwahiyo tunaingia studio tuna vibe. Unajua muziki ni hisia mara nyingi watu wanacomplicate mambo ‘eti wanaandika ngoma wiki mbili sijui wiki moja’ sio kweli sikiliza dude alifu andika vile unafeel.”

Katika hatua nyingine Fid amesema amekuwa akikaa na Chidi kumuweka sawa baada ya hivi karibuni kukamatwa na madawa ya kulevya.

“Hivi ni vitu ambavyo nimeongea naye lakini unajua vitu vingine ni vitu ambavyo wanafamilia huwaga wanaviongea nyuma ya mlango, kwahiyo nisingependa kuviongelea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents