Burudani

Fella: Siwapendelei Chege na Temba ila wao ndio ‘cream ‘ ya TMK

Kiongozi wa kundi la Wanaume TMK, Said Fella amesema dhana ya kuwa yeye huwapendelea zaidi Chege na Temba kuliko wasanii wengine wa kundi hilo si ya kweli.

c5f95b16290c11e3a9dd22000a9e29a7_7

Akiongea na Kali za Bomba, Bomba FM, Mbeya, Fella alisema kama wimbo wa kundi hilo ukitoka bila sauti za wawili hao, hauwezi kufanya vizuri.

“Wale ukiwaona ndio cream ya TMK, ukisema ngoma iwe bila Temba na Chege, hamna ngoma,” alisema.

Alisema kama angekuwa na upendeleo asingeweza kumrejesha kundini YP ambaye alipumzishwa kwa ukosefu wa nidhamu.

“Huyo YP mimi alivyoondoka alivyotukana yale matusi kama mnakumbuka wote watu wa media, nisingemrudisha na asingesikika sasa hivi kwenye ngoma hii ‘Tunafurahi’, kwahiyo hiyo ni dhana potofu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents