Burudani

Fella apanga kuzungumza na Nature wafanye tena kazi pamoja

Said Fella amedai kuwa na mipango ya kuzungumza na Juma Nature ili waanze tena kufanya kazi pamoja.

Maneja wa kundi la mkubwa na wanae pamoja Wanaume family Said Fella akikabidhi msaada kwa wahusika wa hospital hiyo

Fella aliiambia 255 ya XXL, Clouds FM kuwa kuna kila sababu ya kuweka mambo sawa na msanii huyo nguli maisha ya kazi yaendelee kama zamani.

“Huo ni mapango wangu mimi, kwa sababu mimi ndo nafikiria, kama ilitokea wakati ule misunderstanding, kama tulishawishiwa ili tusifanye kazi bana imefika wakati lazima kusameheana,” alisema Fella.

“Mimi nimefikiria nimeona nitakaa na mwanangu nimfahamishe jinsi gani tufanye kazi ili na yeye arudi tufanye kazi. Kuongea tunaongea na mambo muhimu tunashirikiana ila kwenye suala la kazi ndo hilo kwamba nimefikiria ni lazima Mheshimiwa Temba, Chege, na yeye Juma Kassim Kiroboto lazima wakae pamoja wafanye ngoma moja kwanza,” aliongeza.

Fela alidai kuwa chanzo kikubwa cha ugomvi kati ya Nature na wasanii wengine wakiwemo Temba na Chege ni mwanamke.

“Tatizo wote tulivurungwa na ujana mwisho wa siku tukatoa chance kwa watu na wamechukua nafasi. Siwezi kusema sio au ndio, lakini huyo mwanamke ameshinda ametushawishi mpaka kubomoa, maana yake ni sawa sawa mwanamke anatumwa kwenda kubomoa nchi. Viongozi kama tunagombania nchi kwaajili ya mwanamke basi tulifeli sisi upande wetu,” alisisitiza.

Bongo5 ilimtafuta Nature kutaka kujua kama yupo tayari kufanya kazi na Fella na kudai kuwa amesikia taarifa za mpango huo.

“Siwezi kusema tunaweza tukafanya kazi au hatutafanyam,” amesema Nature. “Mimi bado sijaongea naye lolote labda mwenyewe ameamua kusema hivyo ilimradi kionekane ni kitu kizuri. Mimi bado nasikia sikia kwamba Fella kaongea hivi na hivi lakini mimi sijasikia na hajanifuata mimi kuniambia habari hizo. Siwezi kulizungumzia kwa sababu litakuwa linanichota mawazo yangu wakati yeye mhusika hajaniijia.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents