Burudani

Fella anogewa na taarab

Fella_face

Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella ama mkubwa na wanawe, siku mbili hizi anatarajia kuachia ngoma yake mpya ya Midomo Imewashuka ikiwa katika miondoko ya pwani maarufu kama Taarab.

 

Fella hii itakuwa kibao chake cha pili, baada ya kutoka na wimbo wake wa kwanza ambao alimshirikisha mwanadada Isha Mashauzi ‘Jike la Simba’ na kuona umefanya vizuri katika medani ya nyimbo za taarab.

Amesema kwa sasa anadondoka na kijana Hassan Kumbi, ambaye anatoka katika bendi ya Mkubwa na Wanawe itakayotumbuiza katika tamasha la fulamu Zanzabar ZIFF, chini ya Produza Fresh wa Poteza Record.

Aidha fella amesma baada ya kuona anafanya vizuri katika medani ya muziki wa taarab, sasa anakuja na albamu kaajili ya muziki huo na wapenzi wa muziki wake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents