BurudaniWema Sepetu

Fedha ni chanzo cha kuvunjika kwa urafiki wa Wema na Kajala

Mwaka mmoja uliopita, Wema Sepetu aligeuka kuwa shujaa wa maisha ya Kajala Masanja baada ya kujitolea kumlipia shilingi milioni 13 zilizotakiwa kutolewa kama sehemu ya hukumu ya muigizaji huyo ama kwenda jela miaka saba.

Kajala yuko huru. (theTZA millardayo.com )_7
Wema akiwa na Kajala baada ya kumlipia faini yake ya shilingi milioni 13 na kumfanya aachiwe huru

Kitendo hicho kiliwafanya wawili hao kuwa sio tu marafiki bali kama ndugu. Hata hivyo urafiki wao uliianza kuingia doa miezi ya hivi karibuni chanzo kikitajwa kuwa ni ukosefu wa fadhila kwa Kajala dhidi ya rafiki yake Wema ambaye sasa anadai kujutua kumlipia fedha hizo.

Kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya na Global Publishers, moja ya mambo yaliyomvunja moyo Wema, ni kitendo alichomfanyia saa chache kabla ya uzinduzi wa filamu ya Kigodoro na yote yalifanyika kwenye salon moja ya Kinondoni.

“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele, nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno yalishaanza kuwa mimi na Kajala tuna bifu, nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye. Kweli nilipiga makelele ya furaha nilivyomuona K, nikawa nakimbia kwenda kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema nooo…Wema usinikumbatie na kuanza kutoa maneno ya dharau eti nitamchafua. Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi, basi huwezi kuamini, nilishindwa kujizuia nikajikuta namtukana, sikumbakisha. Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe, huwezi amini hali ya hewa iliharibika ghafla kwani sikuwa na mudi tena,” Wema alisema kwenye mahojiano hayo.

Drama ya pili iliyotia dosari urafiki wao, ilitokea kwenye safari yao ya Arusha walikoenda kwenye show ya Mirror. Wema amedai wakiwa njiani, yeye alikuwa hana fedha taslimu za kutosha zaidi ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti hivyo alimwambia Kajala ampe shilingi laki tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani pamoja na matumizi madogomadogo. Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.

“Tulipofika Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue fedha alizokuwa nazo akamuwekee benki kwa sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa eti nilijishaua kuandaa shoo nikitegemea fedha zake. Wakati K anazungumza hivyo kulikuwa na watu watatu, mimi sina hili wala lile nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni, wamekwenda wapi? Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu themanini, kiukweli iliniuma sana, Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa bali alinikopesha? Nilijiuliza amesahau mimi nilitoa Sh. milioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka saba? Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare, viatu sare, mapochi sare, ninachokula na kunywa mimi ndicho hichohicho. Siku zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu nilikuwa ni mimi, leo laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima ananitangazia kwa watu (anataja jina la mwandishi)? Iliniuma sana basi palepale, nikaenda benki nikatoa Sh. milioni mbili, nikamlipa fedha zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote kinachoendelea kwani ningefanya chochote ningeharibu shoo na isingekuwa na maana yoyote ya sisi kwenda Arusha.”

Wema amesema tukio jingine lililomfanya autie mashaka urafiki wake na Kajala ni pale walipopanga kufanya filamu moja na Kajala kubadilika katika hatua za mwisho hali iliyomfanya Wema aamue kufanya na Aunt Ezekiel. Awali wote walikuwa wamekubali kuchangia shilingi milioni 5 kila mmoja.

“Tukiwa katika maandalizi ya mwisho tuanze ku-shoot, K alinipigia simu akaniambia hawezi ku-shoot kwani alikuwa na safari ya kwenda China labda wa-shoot vipande vyake, nikamwambia basi aende akirudi tutatengeneza nyingine.
“Baada ya kuona hivyo ndipo nikamchukua Aunt tutengeneze filamu. K alipoona nimemchukua Aunt, akanipigia simu na kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza mbona mwenzangu amesahau ghafla wema wangu niliomtendea au kwa kuwa tangu aanze vijisafari vyake vya kwenda China anapata.”


Chanzo: Global Publishers

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents