Bongo Movie

Faiza kuja na kipindi cha runinga cha mikasa inayowakuta watu katika maisha yao

Msanii wa filamu Faiza Ally baada ya kukwama kwa kipindi chake cha reality show ambacho kilipangwa
kiruke katika runinga ya EATV, ameweka wazi mkakati wake mpya wa kuja na kipindi kipya cha runinga ambacho kitakuwa kinazungumzia mikasa mbalimbali ambayo inawakuta watu katika maisha yao.
Faiza Ally

Muigizaji huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja aitwae ‘Sasha’ ameiambia Bongo5 kuwa baada ya kuwa muwazi wa maisha yake katika mitandao ya kijamii kumemfanya apokee malalamiko mengi yanayowakuta watu katika jamii hali ambayo imemfanya aanzishe kipindi chache cha runinga ili kuwasaidia.

“Kila kipindi cha zamani cha reality show kilikufa kama watu walivyosikia lakini huo sio mwisho wangu wa kupambana, kuna kipindi kipya kinakuja kuhusu maisha ya watu pamoja na mikasa ambayo wanapitia katika maisha yao,” alisema Faiza.

Aliongeza, “Huwezi kuamini kushare katika mitandao ya kijamii changamoto zangu nilizopitia kwenye maisha kumewafanya watu wengi kujiami na kuniomba ushauri katika mambo yao mbalimbali ya maisha na wengine wanaomba msaada, kwa hiyo nikaona njia sahihi ya kuwasaidia wengi ni kuanzisha kipindi ambacho kitawapa fursa watu kuzungumza mambo mbalimbali ili wapate msaada, kwa sababu kuna wajane wanadhurumiwa mali zao, yaani kuna matukio mengi sana ambayo tukiwapa nafasi watu yakuyasikia wengi watasaidiwa na wengine pia watajifunza,”

Katika hatua nyingine muigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa filamu yake mpya ‘Baby Mama Drama’ ambayo itaingia sokoni mwezi wa sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents