Burudani

Fainali za shindano la Dansi 100% ni Jumamosi hii

Kinyanganyiro cha shindano la kukata na shoka la dansi 100% ambalo limekuwa likiendelea kwa kushirikisha makundi mbalimbali vya sanaa chini ya uandalizi wa kituo cha EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania linafikia kileleni hapo kesho ambapo makundi matano(5) yatachuana vikali katika kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni tano(5) ziotakazokabidhiwa na wadhamini wakuu wa shindano hilo.

001.DANCE
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kutangaza fainali za shindano la Dance 100% litakalofanyika kesho katika Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam ambapo kundi litakaloshinda litaondoka na kitita cha shilingi Milioni tano toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania,Shindano hilo limeandaliwa na EATV

Makundi ambayo yatawasha moto kwenye uwanja wa Don Bosco Oysterbay hapo kesho ni Team Makorokocho, Best boys kaka zao,The winners Crew,Team ya Shamba na The W.D.

Akiongea kuhusiana na fainali hizo Mratibu wa shindano hili, Happy Shame alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya mchuano huo yamekamilika na fainali zitakuwa na mchuano mkali kwa kuwa makundi yote yanayoshiriki ni mazuri na yamejiandaa ipasavyo na kundi litakaloibuka kidedea na ushindi litajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5 kutoka Vodacom Tanzania.

“Tunatarajia fainali zitakuwa na msisimko mkubwa kuwa wasanii wanaoshiriki ni wazuri na tunafurahi mwaka hadi mwaka ubora wa shindano hili unaongezeka na kuwavutia watu wengi wakiwemo wapenzi wa muziki wa dansi nchini,Alisema shame.

Kwa upande wake Matina Nkurlu, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hili alitoa wito kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi katika fainali hizo kuwaunga mkono madansa hao na kuchagua kundi moja wapo ili waweze kufanya nao kazi siku za usoni.

“Shindano hili haliwahusu madansa na vijana peke yake bali watu wote wakiwemo mapromota wanakaribishwa kuja kushuhudia na kuweza kuwashika mkono vijana hawa ili waweze kujituma zaidi katika kazi yao hii ya kudansi wanayoitolea jasho ikiwa ni moja ya ajira kubwa kwa vijana wetu,”alisema Nkurlu.

Alisema kuwa sanaa ikitiliwa mkazo na kufanyika kwa umakini itawawezesha vijana wengi kujiajiri na kujipatia mapato ya kuwawezesha kuendesha maisha yao vizuri, “Vodacom tayari tunatambua kuwa sanaa na michezo inaweza kuinua hali ya maisha ya vijana kwa kupunguza tatizo la ajira ndio maana kampuni imejikita kudhamini mashindano mbalimbali ya sanaa ikiwemo shindano hili la Dansi 100% na daima tutaendelea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na tatizo la ajira kwa vijana.

Alisema ushahidi upo wa vijana wengi hapa nchini ambao miaka michache iliyopita hawakuwa na maisha ya uhakika lakini hivi sasa wanaendesha maisha yao vizuri kutokana na kazi za sanaa wanazozifanya baadhi yao wakiwa ni wanamuziki na wengine wachezaji wa michezo mbalimbali.

“Baadhi ya sanaa na michezo kama vile kucheza dansi,kuimba nyimbo,kucheza mpira wa miguu,kucheza tenesi,kucheza mpira wa mikono,riadha,mpira wa pete,bila kusahau tasnia ya filamu ambayo wasanii wengi waTanzania wamekuwa na mwamko nayo hivi sasa ni ajira tosha kwa vijana ikifanywa kwa umakini na wadau kuwawezesha washiriki na serikali inaweza kupata mapato kupitia fani hizi,alisema Nkurlu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents