Habari

Fahamu unywaji pombe salama unaoweza kuimarisha afya yako

Kipimo salama na sahihi kwa afya bora cha unywaji wa pombe kinabadilika kutokana na umri. Ongea na mfamasia wako kujua ni kiasi gani ni mahususi kwa afya yako.

Hakuna shaka umewahi kusikia kwamba unywaji wa wastani wa bia moja hadi mbili kwa siku kwa mwanamme husaidia kuimarisha afya yako na kukuepusha na magonjwa ya moyo. Lakini hata kama pombe ni rafiki au adui wa afya yako inategemea na vitu viwili; Hali yako ya afya ya sasa na ni kiasi gani cha pombe unachotumia. Ushauri kwa mtu mmoja mmoja ni mzuri zaidi.

Kwa baadhi ya watu inategemea na aina ya dawa wanazotumia na mambo mengine, utumiaji wa pombe hata kwa wastani inaweza kuwa ni hatari kwa afya yako.
Unywaji wa wastani kwa afya yako. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa watumiaji wa wastani wa pombe wanapunguza hatari ya kupata shinikizo la moyo na kiharusi, kisukari na huimalisha mifupa kwa wazee zaidi ya watu wanaokunywa kidogo sana au wasiokunywa kabisa.

Ninapozungumzia wastani namaanisha vinywaji viwili kwa siku kwa mwanaume na kimoja kwa wanawake. Watu wengine huepukana na unywaji wa pombe kwa sababu ni wagonjwa au sababu anatumia dawa zinazokinzana na pombe. Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako kwani zinaweza kukusababishia magonjwa ya moyo,kiharusi na aina Fulani za kansa ingawaje watumiaji wengi wa pombe huwa wanavuta sigara pia.

Baadhi ya matatizo yanayoweza kukufanya usinywe pombe;

• Kama unatumia dawa zinazosinyaza damu (the blood-thinning medication) warfarin (Coumadin),pombe husababisha tatizo la kutokwa na damu.
• Kama unafanya jitihada za kupunguza shinikizo la damu, hata kama utakunywa bia mbili kwa siku inaweza kupandisha BP yako.
• Unywaji wa wastani husaidia watu wanaohiyaji kupunguza uzito.

Tafiti nyingi zimeonyesha watu wanaokunywa bia mbili mpaka sita kwa wiki wanapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo (cardiovascular disease) zaidi ya watu wanaokunywa zaidi. Watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 wanaume kwa wanawake inabidi angalau wanywe bia moja kwa siku. Bia mbili kwa siku zinaweza zisiimalishe afya yako licha yakuwa sihatari kwa afya yako.

Ni vigumu sana kusema kuwa kiasi fulani ndo sahihi kwasababu tafiti nyingi za kisayansi zinaonesha utofauti kutokana na utofauti uliopo baina ya mtu na mtu na jamii inayowazunguka.

Kama haunywi pombe usijaribu kuanza kunywa kabisa kwa matarajio ya kuimarisha afya yako. Ni vema ukaanza mazoezi, ukila vyakula vya kujenga mwili na matunda na usijaribu kuvuta sigara kabisa. Ukizingatia vitu hivi utaimalisha afya yako kwa kiasi kikubwa.

“Kwa watu ambao hawanywi pombe kabisa, ushauri wangu wasijaribu kunywa kabisa, kwani kuna njia nyingi za kukufanya kuwa na afya bora kuliko kuanza kutumia pombe na kuanza kukubwa na athari nyingi za kiafya zinazosababishwa na matumizi ya kupindukia ya pombe.”

Kiasi sahihi ya pombe kinachoshauriwa kiafya ni kama kinavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo

Vinywaji vingine vya pombe vina nguvu kuliko vingine. Kwahiyo ni vizuri kuangalia ni kiasi gani kinachokufaa kiafya, kwa mfano cocktile zingine unaweza kuona zipo kwenye glasi ndogo lakini kumbe ina nguvu zaidi ya bia tatu mpaka nne.

Your Health, Our Concern

IMEANDALIWA NA:
FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/Pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents