Habari

Fahamu madhara yatokanayo na utumiaji wa dawa za kupunguza uzito

Kwa watu wanaohitaji kupunguza uzito, diet supplements huonekana kama NJIA YA MAAJABU. Na kwakufahamu hilo watengenezaji wake wamekuwa wakiwaahidi watumiaji wake sifa ambazo inawezekana hata hazipo bila hata ya kuwa na uthibitisho mkubwa wa tafiti zake.

Ukiachilia mbali utumiaji wa dawa hizo kutokana na sababu za kiafya kutokana na ushauri wa daktari, unaweza kuiweka afya yako katika hatari kutokana na utumiaji wa dawa hizo.

Nini Maana Ya Diet Supplements?

Diet supplement ni bidhaa yeyote inayomezwa yenye viambato kama vile virutubisho mbalimbali, dawa asilia, na viambato vingine ambavyo huongezwa kwa minajidi ya kuongeza vitu vya ziada katika mlo (diet). Sio supplements zote huwa zinatengenezwa kwa ajili ya kupunguza uzito zingine huwa zinalenga kuongeza vitu ambavyo mtu huvikosa katika mlo wa kawaida

Dietary supplement zinaweza kuwa na viambato vifuatvyo:
• Vitamini
• Madini
• Amino asidi (Building blocks of protein)
• Vimeng’enywa (Enzymes)
• Botanical products/herbs

Ni kwa Jinsi Gani Bidhaa Hizi Hufanya Kazi?

Diet supplements hupatikana katika fomu tofauti tofauti kama vile vidonge, majani ya chai, unga na vinywaji. Bidhaa hizo hutumika pamoja na chakula au badala ya chakula. Bidhaa hizi zinatakiwa kuufanya mwili wako kupunguza uzito kwa kuamsha metabolism ya mwili wako au kuufanya mwili wako kutumia nguvu yakutosha katika kujiendesha. Mfano wa viambato hivyo kama caffeine huamsha mfumo wa fahamu na kusaidia kuchoma fati kwa kutumia njia inayoitwa THERMOGENESIS. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi ya faida.

Kwanini dawa za kupunguza uzito ni hatari kwa afya yako?

Diet supplements nyingi sio hatari , na nyingine hutengeneza hali ya kukufanya ujisikie umeshiba na huvunja vunja fati au kuongeza metabolism kwenye mwili wako. Lakini bidhaa nyingi zina viambato ambavyo mamlaka nyingi zinazohusika na ubora wa bidhaa hizo duniani kote zimepiga marufuku matumizi yake kutokana na madhara yafuatayo;
• Kuongeza mapigo ya moyo
• Shinikizo la damu
• Kuharisha
• Kukosa usingizi
• Kuharibu ini
• Kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa

Ephedra – Diet supplements ambayo inatokana na dawa za asili za kichina iliyopigwa marufuku. Asilimia 64 wamepata madhara kutokana na kutumia dawa hii kutoka na utafiti uliofanyika- WebMD

Hydroxycut –Husababisha magonjwa ya ini, figo, na ogabi zingine muhimu za mwili. Ripoti iliyotolewa na Consumer Reports, inaonesha watumiaji wake wengi wamepata madhara kama Hepatitis na homa za manjano

Fenfluramine-Hutumika kinyume na matumizi yake (off-label diet drug) na kusababisha matatizo ya moyo na mapafu.

Je unakijua kitu Unachokitumia?

Watengenezaji wengi wa dawa hizi huwa hawaainishi baadhi ya viambato walivyoviweka. Njia nzuri yakutambua ni kuomba ushauri wa wataalam wa afya. Vifuatavyo ni baadhi ya viambato vinavyochanganywaga kwenye dawa hizo;-
• Sibutramine: dawa yakupunguza uzito ambayo husababisha shinikizo la damu (high blood pressure), shambulio la moyo (heart attack) na stroke (kiharusi)

• Rimonabant: dawa ya kupunguza hamu ya kula (appetite suppressant) ambayo imepigwa marufuku

• Phenytoin: dawa yakuzuia mshtuko (anti-seizure drug)

• Phenolphthalein: Dawa ya majaribio inayoweza kusababisha kansa (an experimental drug)

Ni kwa jinsi gani dawa za kupunguza uzito zinavyotumiwa vibaya (Abused)?
Kuna baadhi ya watu wana matatizo ya kula (eating disorder) hawawezi kuwa na shaka kutokana na madhara yatokanayo na dawa za kupunguza uzito.

• Wasichana wengi wakishakuwa na dhamira ya kupunguza uzito huwa hawajali madhara yatakayo hatarisha afya zao. Zifuatazo ni njia zisizofaa zinazotumika kupunguza uzito;

• Kutumia dozi zaidi ya ile iliyoelekezwa na mtaalam wa afya

• Kutumia diet products ambazo hazipaswi kutumiwa na watu ambao wana uzito wa kawaida au chini kidogo

• Kutumia dawa za kupunguza uzito ambazo zinapaswa kutumiwa kwa maelekezo maalum ya daktari bila ruhusa ya daktari

• Kuchanganya dawa zaidi ya moja yakupunguza uzito

• Kuchanganya dawa za kupunguza uzito pamoja na dawa za moyo pamoja na dawa zinazotumika kutibu constipation.

• Kuchanganya dawa za kupunguza uzito pamoja na cocaine au meth
Kutumia dozi kubwa au kuchanganya aina tofauti za dawa za kupunguza uzito husababisha madhara makubwa ya kiafya.Kutumia dozi kubwa ya dawa hizi husababisha kuongeza msukumo wa damu kwa kiwango kisichotakiwa na kuababisha shinikizo la damu kupelekea mtu kupata shambulio la moyo na kiharusi.

Kutumia dawa zinazozuia metabolism za fati kutokea pamoja na dawa za constipation na za moyo husababisha kuharisha, kupoteza maji pamoja na kutoweka kwa usawa wa chumvi mwilini (electrolyte imbalance). Pia dawa hizi husababisha ogani mbalimbali kushindwa kufanya kazi (organ failure).

Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa afya yao ni kitu muhimu sana hivyo bhasi ni lazima waongeze umakini kuhusiana na vitu wanavyotumia. Pia mamlaka zinazohusika ni muhimu zikaangalia wimbi hili lililoibuka hivi karibuni la utangazaji holela wa bidhaa hizi za kupunguza uzito bila kufuata utaratibu.

Your Health, My Concern

IMEANDALIWA NA
FORD A. CHISANZA
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]
[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents