Habari

Fahamu kwa undani sakata la kujiuzulu kwa rais wa Guatemala

Masaa machache baada ya rais wa Guatemala, Otto Perez Molina kujiuzalu, alitupwa jela kusubiri kesi yake ya upotevu wa fedha nyingi ambazo zimetikisha nchi hiyo kiuchumi na kanda nzima.

2012198412773734_20

Maamuzi hayo yalifikiwa baada ya maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa toke mwezi wa nne wakimtaka aondoke madarakani na kushtakiwa kwa makosa ya rushwa kubwa. Kitu hicho ambacho kimeshangaza kwa kiasi kikubwa ni nchi ambayo imetawaliwa kimabavu kwa kutumia jeshi na kidikteta lakini rais ameweza kuamriwa kujiuzulu na wananchi na wakati huo huo atapandishwa kizimbani kujibu mashitaka.  

Hayo yote yametokea siku moja ya kujiuzulu na kwenda jela. Hiyo ni historia ya aina yake kutoka ikulu na kwenda kuanza maisha mapya jela kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Rais Otto Pérez Molina aliondolewa kinga yake ya kushtakiwa na bunge la nchi hiyo tarehe 1 Septemba 2015, na hii ilijidhihirisha wazi pale maandamano yalikuwa yakifanyika mitaani hivyo haikuwa rahisi kuondoka madarakani na kwenda kuishi maisha ya amani.

Ingawa rais huyo aliyekuwa mkombozi wao ndiye aliyefanya makubaliano na kuendesha mazungumzo ya kijeshi la nchi hiyo ili kusimamisha miaka 36 ya umwagaji damu. Lakini mwisho wa siku alikubali kuondoka madarakani na kusema yuko tayari kusimama kukabiliana na yanayomsibu katika maisha yake binafsi.

Alhamis hii aliweza kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza wakati mashtaka yake yakisikilizwa ambayo yamemweka matatani, yaliyokuwa yamejaa matukio na mazungumzo yake yanayohusiana na rushwa kubwa ndani ya nchi hiyo.

Ilichukuwa masaa sita kwa majaji na mawakili na vyombo vya habari kusikiliza sauti za kurekodiwa ambazo zinahusisha mazungumzo ya rais huyo aliyejiuzulu wadhifa wake.

Baada ya hapo, alisimama na kuongea na vyombo vya habari akisema hana makosa wala hana hatia yoyote kutokana na mashtaka hayo.

Alisema; Kusikiliza mashtaka ni jambo moja na kufanya uchunguzi ni jambo jingine. Watu wa Guatemala wanatakiwa kuheshimu sheria.

Baada ya Pérez Molina kuondoka hapo mahakamani alipelekwa mahabusu zilizojaa washitakiwa wa makosa ya kihalifu na wengine wanaosubiri kusomewa mashtaka yao. Walipiga kelele na kumuonyesha ishara za kumtishia na maneno ya kumtishia maisha yake. 

Siku ya Alhamisi ilikuwa ni siku ya sherehe na furaha kwa wananchi wa Guatemala baada ya maandamano ya miezi mitano, wakisema mkakati wa kumwondoa rais madarakani umekwisha.

 

04guatemala01-articleLarge
Wandaamanaji hao wakiwa mtaani

Makamu wake, Alejandro Maldonado ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo siku ya alhamisi aada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kukubali kujiuzulu kwa Molina.

Pérez Molina, 64, ni rais wa kwanza kwenye historia ya Guatemala kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa. Hatua hiyo inaifanya nchi hiyo kuwa na siasa za watu ambao wanaweza kuwajibika. Waandamanaji hao walisema hata Maldonado asiposikia sauti zao na yeye pia watamfukuza kwenye kiti hicho mpaka sauti yao isikike  kwenye serikali ya nchi yao.

Najaribu kufikiri ni lini nchi zetu za Afrika tutaweza kufikia kwenye maamuzi magumu kama hayo pale ambapo tunaona rushwa ikitawala? Je Marais wa Afrika watajifunza somo hilo kutoka Guatemala?

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents