Technology

Facebook Pesa? Facebook yadaiwa kuwa na mpango wa kuanzisha huduma za kifedha

Miaka michache ijayo M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money zinaweza kuwa na mpinzani mwingine, Facebook Pesa!!

The loading screen of the Facebook application on a mobile phone is seen in this photo illustration taken in Lavigny

Katika miaka ijayo Facebook haitakuwa sehemu tu ya kuandika status, kupost picha ama kusoma kinachoendelea mjini bali itakuwa sehemu ambapo watumiaji wataweza kufanya malipo ya kieletroniki na kutunza fedha pia. Mtandao huo wa kijamii unadaiwa kuwa kwenye mchakato wa kuingia kwenye utoaji wa huduma za kifedha ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyakazi waliopo nchi za kigeni wanaweza kutuma fedha kwa familia zao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Financial Times, Facebook imetuma maombi kwenye benki kuu Ireland, ambapo kama ikipewa itawaruhusu watu kutunza fedha kwenye mtandao huo wa kijamii, kuhamisha kwa watumiaji wengine na kulipia bidhaa ama bili.

Pia mtandao huo umezungumza na makampuni mapya ya huduma hizo ya London, TransferWise, Moni Technologies na Azimo ambayo yanatoa huduma za utumaji fedha kwa njia ya apps za smartphone.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents