Michezo

FA ya mtoza Bacary Sagna faini ya Paundi £40,000

Mchezaji wa klabu ya Manchester City Bacary Sagna, ametozwa faini ya paundi elfu 40 na shirikisho la soka nchini Uingereza FA baada ya kuandika ujumbe ’10 dhidi 12” akimaniisha kuwa wachezaji 10 dhidi 12 katika mtandao wake wa Instagram kufuatia mechi kati yao na Burnley.

Beki huyo wa kimataifa ambaye ana umri wa miaka 33, kutoka Ufaransa alisema hayo wakati timu yake ilipopata ushindi wa mabao 2-1 katika ligi ya Uingereza Januari 2.

Huu ndio ujumbe alio uandika Sagna

City walipunguzwa na kusalia wachezaji 10 katika dakika ya 32 ya mchezo , pale mwamuzi Lee Mason alipomtoa nje kiungo wa kati Fernandinho kwa kumpa kadi nyekundu.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limesema katika taarifa, hiyo ambayo baadae ilifutwa kwamba chapisho hilo lilihoji uadilifu wa mechi hiyo.

Sagna pia ameonywa kuhusu mwenendo wake.

City hatahivyo haijaondoa uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya faini hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents