Burudani

Exclusive: Sheddy Clever aeleza jinsi ‘zali’ la kumrekodi Ne-Yo na Diamond lilivyomdondokea

Wapo watayarishaji wengi na wazuri wa muziki nchini Tanzania, lakini Sheddy Clever wa Burn Records ndiye aliyebahatika kuchaguliwa na Diamond Platnumz kwenda Nairobi kusimamia zoezi zima la kurekodi collabo ya kimataifa ya Diamond na Ne-Yo kutoka Marekani.

sheddy na Ne-yo

Bongo5 imemtafuta mtayarishaji huyo wa ‘Number One’ na ‘Ntampata Wapi’ zote za Diamond, ambaye ametueleza jinsi alivyojikuta akitimiza ndoto ambayo hakuwahi hata kuiota, ya sio tu kukutana bali kumrekodi mshindi wa tuzo za Grammy Ne-Yo kwenye beat aliyoitengeneza.

“Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwasababu yeye ndiye muweza wa yote, pili naushukuru uongozi wa WCB kwasababu wao ndio wamefanikisha haya yote. Kwakweli nimejisikia furaha sana kwasababu sikutegemea kama nitakuja kufanya kazi hii.” Alisema Sheddy.

Sheddy alianza kwa kuelezea jinsi ilivyokuwa mara ya kwanza anapigiwa simu na Diamond kupewa dili hiyo;

“Mi nimepigiwa tu simu na Diamond akaniambia kuna kazi inatakiwa ifanyike kwahiyo tunatakiwa kusafiri, nikamwambia poa nashukuru, na akaniambia kila kitu tiketi yako ipo jiandae kwa safari… basi tukasafiri tukaenda tukafanya hiyo kazi…nashukuru Mwenyezi Mungu. Ni kazi nzuri na naimani itafika mbali.”

nnnn

Katika wimbo huo wa Diamond aliomshirikisha Ne-Yo, yeye Sheddy Clever amehusika kwa kiasi gani?

“Nimetengeneza beat, na vocal za Diamond kila kitu yaani nimeutengeneza wimbo kwa ujumla, Ne-Yo yeye tulimfata kule kwaajili ya kuweka vocal zake, Beat tulitengeneza pale studio (Nairobi), studio ile Diamond alilipia kwahiyo nilikabidhiwa studio kila kitu, ila kulikuwa na producer wake na Ne-Yo ni mzungu pia ndiye ambaye tulikua tunashauriana naye kubadilishana mawazo na nikajifunza vitu vingi zaidi.”

Tupe uzoefu wako wa wakati unamrekodi Ne-Yo akiwa booth, ni msanii wa namna gani?

“Ne-Yo kwanza ni mtu mmoja amabye yuko peace sana tofauti na nilivyokuwa namfikiria, japokuwa nilikuwa na uwoga pia nikasema hivi ntamwambia nini hivi akikosea ntaweza kumrekebisha kweli? Lakini Ne-Yo anapenda pia kurekebishwa anapokosea, na anapenda pia ushauri sana kila anachokifanya anauliza niko poa? Vitu kama hivyo.”

Ilimchukua muda gani Ne-Yo kurekodi sauti?

“Kwa upande wake hatukusumbuana sana nafikiri tulipiga kama take mbili tu akamaliza kurekodi kwasababu ana uzoefu wa siku nyingi.”

Ne-Yo anazifahamu kazi ambazo umetengeneza zikiwemo za Diamond?

“Yeah Diamond alimwonesha kazi zote ambazo nimefanya na anapenda sana wimbo wa Number One.”

Sheddy ambaye pia anawania tuzo ya Producer wa Muziki Wa Mwaka kwenye tuzo za AFRIMMA 2015,amemshukuru Diamond kwa heshima ambayo amempa kwa kufanya naye kazi na kumkutanisha na wasanii wengi wakubwa.

“Diamond amenipa heshima sana , kufanya nae kazi na kunikutanisha na wasanii wengi tofauti kwahiyo hii ni heshima kwangu, najiona nimekuwa tofauti na nimekuwa mkubwa…” alimaliza Sheddy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents