Burudani

Exclusive: Rama D ataja jinsia ya mtoto wake na siku atakayozaliwa, arudi shule, aukubali wimbo wa Hisia ‘Mawazo’

Rama Dee aka Baba Abiguel amesema mtoto wake ajaye atakuwa wa kiume na anatarajiwa kuzaliwa siku moja aliyozaliwa yeye, July 3.

IMG-20140215-WA0003

“Natarajia kupata mtoto mwingine ambaye atazaliwa siku sawa kabisa na siku yake ya kuzaliwa. Mtoto ni wa kiume so nipo na furaha sana,” Rama Dee ameiambia Bongo5. “Kama ikiwahi zaidi ni mambo ya Mungu maana hutokeaga matatizo ya wanawake kwenye mambo ya uzazi.”

Kuhusu muziki, Rama Dee amesema kwa sasa amesimama kwa muda.

“Nimesimama kidogo maana nipo kwenye masomo. Naona nitulie kidogo. Kwa sasa nimesimama hata kutumia Twitter na Facebook kwa muda ila nipo vizuri tu,” amesema muimbaji huyo wa ‘Kama Huwezi’.

Katika hatua nyingine, Rama Dee amesema amefurahishwa na nyimbo mpya za wasanii wa Tanzania zilizotoka mwezi huu.

“Nasikia raha sana kuomba waimbaji wameanza kujitokeza. Kuna jamaa anaitwa Hisia, atakuja kuwa vizuri sana baadaye. Nimependa wimbo wa Hisia. Zaidi amepanga vizuri sana sauti halafu nimeona kitu kikubwa sana kwake. Yupo na kipaji jamaa. Wabongo watachelewa kumwelewa ila wakimwelewa itakuwa daima,” amesema.

“Ben Pol released a good song but he didn’t finish the song. It seems like he was still writing his verses and rushed the released. Namkubali sana ila naangalia uwezo wake kama hajaupa nafasi ya kutosha, alitakiwa amalize hizo verses zake, ni mtazamo tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents