Bongo5 MakalaBurudani

Exclusive: P-Funk azungumzia ujio wa album mpya ya Ngwair, album yake, kubadili jina, studio mpya na kuanzisha shule ya sound engineering

Producer P-Funk Majani amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu msiba wa Ngwair mwezi May mwaka jana. Hata hivyo ukimya wake haukuwa wa bure kwakuwa Godfather huyo wa Bongo Flava alikuwa akiidhatiti ngome yake ya Bongo Records na sasa kupitia mahojiano ‘exclusive’ na Bongo5, Majani amefunguka kwa urefu kile anachokifanya kwa sasa.

DSCF-620x342


Kuhusu kwanini alikuwa kimya tangu tangu msiba wa Albert Mangwea

Baada ya mazishi ya Ngwair tulianzisha chama cha maproducer kilikuwa kinaitwa TSPA (Tanzanaia Sound Producers Association) na mimi nilikuwa mwenyekiti wa hiyo. Lakini tulienda tukakuta baadaye inafeli so tukaibadilisha kutoka chama ambacho kilitakiwa kisajiliwe chini ya home affairs, tukaanzisha kampuni ambayo inaitwa TSPL (Tanzania Sound Producers Limited) ndio tunahangaika nayo sasa hivi ambayo itakuwa na maproducers wote chini ya hiyo kampuni.

Kwa ufupi kuhusu Bongo Records, nafanyafanya kazi na watu wangu ambao nawafahamu akina Jay Mo kuna ngoma kibao, akina Profesa Jay tumefanya vitu vipya, Stamina na MB Dogg naye anatakurudi halafu na chipukizi ambao bado hamuwafahamu ndio tunatoka nao. Lakini my main interest kutoka sasa hadi mwezi wa sita kuna album mbili naziandaa. Kuna album ya marehemu (Ngwair) ambayo inatoka ambayo itakuwa na nyimbo nane ambayo itakuwa inashirikisha wasanii tofauti.

Halafu pia kutakuwa na album ya mkusanyiko inatoka ambayo ni ya kwangu. Mimi ntakuwa naimba labda na Godzilla, Godzilla ndio ataandika nyimbo. Mimi ntaimba mashairi yale ya Godzilla labda verse moja, nyingine ataandika Joh Makini, ataimba na mimi ntaimba verse moja hivyo hivyo. Kwasababu kwa siku zote mimi naweza kuchana na kila kitu lakini kuandika kwa Kiswahili kupata mashairi mazuri huwa nashindwa. Kwahiyo ntakuwa nawatumia wataalam wa muziki wa hip hop wa Bongo Flava ili tuweze kuandaa kitu kama hicho.

Sioni umuhimu siku hizi kutoatoa nyimbo hivyo redioni, nyingi zinapotea tu. Ni bora tufanye kazi imara lakini chache lakini sio nyingi lakini hazina longevity, hazidumu. Ila mwaka huu nimesema kila mwezi walau nitoe wimbo mmoja. Kwa mwezi wa January ilikuwa ya Profesa sema ameichelewesha sababu wanataka kushoot video kwanza. Halafu mwezi wa February anatoka Jay Mo na Ommy Dimpoz. Halafu March inatoka single ya kwanza ya Albert. April natoka mimi single yangu ila sijui na nani kama nina Profesa, Joh Makini, Godzilla ama Fid Q, bado sijui.

Halafu kingine siku hizi unajua nafanya matangazo mengi ya redio, so niko busy na hivyo pia. Zinalipa zaidi ya kurekodi.

Bongo Records tumeikarabati toka mwaka jana. November nilienda Ulaya, nimenunua vyombo Ujerumani so we have new equipments, we have new studio. It’s beautiful hadi mimi mwenyewe nasikia raha kufanya kazi siku hizi. Ni kama mtoto mdogo amepata toy mpya. So mzuka wa kazi ya muziki ninao. Sasa hivi pia tuna platform ni umoja wetu unatusaidia kidogo kulindalinda haki zetu, unajua unafanya kazi kwa amani, unajua kabisa. Kuna jinsi ya kudhibiti kuhakikisha kuwa maslahi yanatufukia sisi wahusika. Na hilo ni jambo kubwa ambalo lilinifanya mimi nisirekodi kwa miaka iliyopita sana. Nilikuwa naona, yeah narekodi nyimbo, nazitoa redioni lakini napataje faida mimi? Lakini msanii ataenda ataimba kwenye show. Mimi ntapataje advancement yoyote?

Kuhusu majina ya album ya Ngwair na album yake ya mkusanyiko

Ya Ngwair nadhani kwakweli tutatumia wananchi kuitafutia title. Tutafanya labda kampeni redioni, ikishakaa vizuri na tuhusishe wananchi kwenye blogs, social media na broadcasts hizi za kawaida. Kusema ukweli we don’t have a title yet.

Ya kwangu, cha kwanza kinachochekesha kwenye kufoka nimebadilisha jina. Mimi kwenye kufoka ntakuwa najiita Dream Big. Dream kuota, Big ni kwamba uwe na ndoto kubwa. Usiwe unafikiria vitu vidogo maishani, ota ndoto kubwa. And the whole initial plan is,mimi mwisho wa siku I always had a dream making it across Africa. Mungu amenipa kipaji ambacho unajua naweza kuchana Kiingereza, naweza kuimba ila sasa Kiswahili kinanipiga chenga na mimi ili kuonesha natokea Tanzania, nahitaji pia elements za Kiswahili. Lakini pia ili kuweza kufika Afrika lazima nijenge heshima, hapa ndio ninaheshima ya production lakini sio ya kuimba mimi. Nijenge heshima nyumbani halafu nianze kuvuka mipaka sasa pole pole.

Ndio maana naanza na kila Godzilla, ili nifanye kwanza hizi projects nianze kukubalika hapa, Kenya, Uganda halafu pole pole naweza kuingia kwenye Kiingereza kitupu and so on. Lakini hata nikipiga Kiingereza, instrumentation inakuwa ya Kiafrika zaidi inakuwa hip hop African fulani ambayo hata Mmarekani akiskiliza atasema ‘what the hell is this’. So najipanga, nipo gym najaribu kukata weight kuwa na muonekano wa kisanii.

Kuhusu kama utayarishaji wa muziki wa Tanzania umekua ukilinganisha na nchi kama Nigeria

Production wise siwezi kulalamika kabisa, watu wanatengeneza beats nzuri ila kwenye failure kidogo ni the final .. the mixing, the engineering, the technical. Kuna wachache ambao wanafanya vizuri ambao nasema ‘these guys are doing good’ na wengine fifty fifty na wengine ambao wanahitaji support. Ndio maana nataka kufanya course ya Sound Engineering hapa studioni kwangu ntakuwa nachukua maproducer sita kwa mwezi. Kila darasa linakuwa na wanafunzi sita, somo ni mara nne kwa wiki, kwa mwezi inakuwa masomo 16. So nilishapata maombi mengi, maproducer wengi walishaniambia lakini I was trying to advance it first. Hiyo ada yake yenyewe sio gharama, ni laki 5.

Sikiliza sauti ya mahojiano hayo hapa:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents