Habari

Exclusive: Kili wajibu baadhi ya malalamiko ya wasanii waliokosa nominations kwenye tuzo

Tangu kutajwa kwa majina ya wasanii watakaowania tuzo za muziki za Tanzania mwaka huu, Kili Music Awards, kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasanii waliodai kutotendewa haki na academy iliyopitisha majina kwa kutozitaja nyimbo zao licha ya kuamini kuwa zilifanya vizuri.

IMG_7426

Miongoni mwa wasanii waliolalamika ni pamoja na TID na Hussein Machozi wanaodai kuwa ‘Kiuno’ na ‘Addicted’ zilitakiwa kuwepo kwenye orodha ya nyimbo zitakozoshidania tuzo mwaka huu.

Malalamiko mengine yanahusu Diamond kutajwa kuwania vipengele viwili tu licha ya nyimbo zake kuendelea kufanya vizuri. Kuliwahi kuwepo pia tetesi kuwa Diamond na waandaji wa tuzo hizo walitofautiana kauli mwaka jana.

Bongo5 imezungumza na mmoja wa wahusika wa mchakato huo na wanaosimamia tuzo hizo, aliyejibu kwa niaba ya meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe ambao ni wadhamini wa tuzo hizo.

Kuhusu suala la Diamond

Kaingia kwenye category mwaka huu kwingine kote hakufit kwa mwaka jana. Kwa mwaka ujao pengine anaweza akatokea zaidi cause I think kazi zake za mwaka huu zimefanya vizuri zaidi.
Wakati academy inakaa hakuna rules zinazotolewa na Kili labda ‘Diamond asiwepo, TID asiwepo, hakuna. Watu wanapiga kura kwa mujibu wa kazi zilizofanya vizuri kwa msimu wa Kili.

Hakunaga shortlist nyingine zaidi ya shortlist waliyoifanya wenyewe, unless Diamond amegombana na academy nzima. Lakini otherwise kwenye category kaingia ndivyo academy imeonelea anastahili kwa mwaka jana.. Kwingine alitokea akapata kura moja kura mbili akazidiwa na wengine. Kingine hata ukiangalia category zilizopo, umtoe nani umweke Diamond. Hata ukiangalia tu mwaka huu ambao unasimamiwa sasa hivi na Kili he didn’t perform that well kwa mujibu wa academy, ni hisia tu.

Kuhusu malalamiko ya Hussein Machozi

Hata mtu yeyote ambaye anafuatilia ukimwambia ataje nyimbo tano za RNB mwaka jana, Addicted ataisahau so it’s not personal, kura zake hazikutosha tu, watu hawakumchagua, hawakudhani kama alifanya vizuri mwaka jana, same thing to Diamond yaani sio kwamba kuna watu wanakuwa handpicked. No. What I am seeing here now which is not good at the same time kwasababu inaweza hata ikawaharibia watu wengine wakubwa.

We can discuss na watu wa Innovax if they feel kwamba it’s okay kupublish zile kura za academy utaona kuna majina mengine yametokea huku moja, mbili tatu nk lakini kuna wimbo mwingine una kura zote hamsini yaani academy nzima imempa kura.

Kuhusu kuwepo malalamiko mengi kuhusu tuzo za Kili

Kutokuwa na malalamiko I don’t think it will ever happen, again kwasababu tuzo zinadeal na hisia za watu. Msanii amefanya kazi yake ameamini imefanya vizuri, kweli inaweza kuwa imefanya vizuri lakini kuna kazi zingine zimefanya vizuri zaidi yeye haoni hilo, atalalamika.

Kwahiyo that will always happen no matter how tuzo mfumo wake utajitahidi uuperfect mchakato kwa kiasi gani that’s not gonna go away lakini I can tell you kwamba hawa watu 50 wanatoka kona tofauti, hawajuani kama wako kwenye academy. They come and they meet pale na kuanza kazi. Halafu it’s normally very tight yaani huwa hakuna hata muda wa kusema ‘kikundi hiki kikae., kiamue tumpitishe huyu. Ukipita pale kwasababu academy imeamini you were good mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents