Burudani

Ernest Napoleon aelezea kwanini alitumia wimbo wa Ngwair kwenye soundtrack ya Going Bongo (Video)

Muigizaji wa filamu ya kwanza Afrika Mashariki kusambazwa kupitia mtandao wa iTunes, Going Bongo, Ernest Napoleon ameelezea kwanini aliishawishi kwa nguvu zote timu iliyotayarisha filamu hiyo kuujumuisha wimbo wa Ngwair, Nipeni Dili kwenye soundtrack yake.

https://www.youtube.com/watch?v=-_qxjihURHA

Ernest ambaye pia hujulikana kama MC Napo, amesema timu hiyo ilikuwa imependekeza kutumika kwa wimbo wa Afrika Kusini katika scene iliyohitaji wimbo unaokimbia.

Hivi ndivyo anavyoelezea:

Kabla sijaondoka Bongo kuelekea Marekani, nilikuwa nafanya Bongo Flava. Moja ya ndoto zangu ilikuwa kuifikisha Bongo Flava internationally. Kipindi kile kusema ukweli, hakukuwa na msanii ambaye alikuwa na nafasi ya kufanya hivi. Miezi michache kabla sijaondoka, nilisikia nyimbo mpya iliyoitwa “Ghetto Langu” ya Mangwea.

Baada ya kutoka kwa nyimbo ya “Ghetto Langu”, nilianza kukutana na Mangwea katika matamasha mbalimbali na kubaini uwezo wake mkubwa wa kubalance lyrics na style ya kuimba nakumbuka tulifreestyle pamoja pale Clouds FM kabla ya show ya Juma Nature ya Ugali kama sikosei ambapo alifunika wasanii wenzake vibaya mno.

Miaka mingi ilipita baada ya mimi kuondoka Bongo, lakini niliendelea kufuatilia muziki na career ya Mangwea. Kwangu mimi niliona ni msanii ambaye angetutoa kimataifa kutokana na kipaji alichokuwa nacho.

Karibu 90% ya nyimbo zake zilikuwa nzuri sana.

Wakati natengeneza Going Bongo, nilikuwa nasikiliza sana Bongo Flava. Hii nyimbo ya Nipeni Deal ilikuwa kwenye playlist yangu na ilikuwa ni nyimbo ambayo niilipenda sana. Baada ya hapo nikapata wazo la nilikuwa nataka iwepo kwenye filamu ingawa watu wengi walisuggest nyimbo nyingi za South Africa zilizokuwa katika beats ya aina hiyo.

Baada ya kushikilia uamuzi kwamba hii nyimbo ya Mangwea lazima iingie kwenye hii movie, nilianza kuwasiliana naye upya baada ya kipindi kirefu. Tulianza mazungumzo ya kutumia nyimbo hiyo siku chache kabla ya safari yake ya South Africa. Kwa bahati mbaya hiyo ndio ilikuwa safari yake ya mwisho. Natumaini watu watakaopata kuingalia Going Bongo, wataenjoy scene ya disco ambayo nyimbo hii ilitumika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents