Burudani

Exclusive: Diamond azungumzia tetesi za kupanga kumuoa Meninah ‘nahuzunishwa sana’

Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah Atick.

10464206_763180223703794_2359589105802256374_n

Diamond ameiambia Bongo5 kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.

“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema msanii huyo. “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua kabisa siwezi kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua utaongea na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa kimya,” ameongeza Diamond.

wema
Wema

“Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi mie nataka kumuoa Meninah’ Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah. Kila mtu anajua mie nina mahisiano Wema. Wema ndo mpenzi wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu hawawezi kumchukia! Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti.”

meninah
Meninah

“Unajua kitendo hicho hatamaye kinaniudhi naona mtu yupo na mpenzi wake halafu anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila mtu hakimpendezi. Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kupitia njia hiyo. Labda wana wasanii wao, sasa wanaona tukiingia kwa njia hii tutaweza kuamharibia Diamond. Ndioa siku zote nimekuwa kimya tu ila sina mahusiano na Meninah. Mie nikiwa na mtu huwa sifichi naweka wazi kabisa. Hata kama leo nimeachana na Wema nasema tu, why nifiche? Mie katika mambo yangu huwa simuogopi mtu kama ningekuwa nataka kuoa basi ninge weka wazi why nifiche?”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents