Burudani

Exclusive: AY atoa ujumbe muhimu kwa mashabiki na marafiki katika siku yake ya kuzaliwa leo

Leo ni siku ya kuzaliwa ya miongoni mwa wasanii wachapakazi na wanaojituma zaidi Afrika Mashariki, Ambwene Yesaya aka AY.

IMG_9837

AY ambaye mwaka jana alishinda tuzo ya video bora ya wimbo wa Afrika Mashariki, I don’t wanna be Alone kwenye tuzo za Channel O, ameongea na Bongo5 asubuhi ya leo na kutoa shukrani zake nyingi kwa mashabiki na marafiki wanaoendelea kummininia salamu tele za pongezi.

“Ninawashukuru tu, unajua ujumbe ni mwingi mno nashindwa hata kujibu kila mtu, ukiangalia Twitter yangu ina followers 50,500 sasa hivi. Nilijaribu kujibu jana lakini nikachemsha kwasababu watu wanakuwa na attention, tuongee tufurahi pamoja lakini nawashukuru sana kwa kunitakia heri, nawapenda wote na tuendelee kuwa pamoja, tuendelee kufanya kazi,”amesema AY.

Amesema marafiki wa nje wakiwemo meneja wake Henry Kiwanuka na mwanamuziki wa Marekani, Lamyia Good aliyewahi kumshirikisha kwenye wimbo wake, Speak With Your Body walimuomba aende Marekani kufurahi nao lakini amesema awamu hii ataitumia siku yake ya kuzaliwa kufurahia na watu wa nyumbani.

Kuhusu ratiba yake ya siku ya leo, AY amesema kama siku zote lazima aende kwenye kaburi la mama yake (RIP) kumwombea kabla ya mambo mengine.

“Baadaye labda nikishamaliza makaburini nikipata lunch ntachukua boti, nizungukeee, baada ya hapo nijisalimishe kwa kamati kuu ya ndoo, unajua mimi ndio nilianzishaga mchezo wa ndoo sasa wataniua wale, wana hasira haoo.”

Katika hatua nyingine AY amesema yeye na mchumba wake wanapishana siku mbili tu za kuzaliwa.
“Tumepishana siku mbili tu, yeye kesho kutwa , so tuliongea tu kwenye simu jana. Ilikuwa tuwe pamoja lakini ratiba… yaani kusema ukweli itabidi na yeye anisamehe tu.”

IMG_9993
AY akiwa na mchumba wake (May 1, 2013)

Tunamtakia AY birthday njema na furaha tele siku ya leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents