Burudani

Ex wa Nicki Minaj afikiria kujiua baada ya kupigwa kibuti!

Aliyekuwa boyfriend wa Nicki Minaj ameumizwa na kitendo cha kupigwa kibuti kiasi kwamba anafikiria kujiua.

Nicki Minaj Album Signing For "Pink Friday: Roman Reloaded"

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Safaree Samuels amewaambia washkaji zake kuwa ameumizwa na kuvunjika kwa uhusiano wake wa miaka 12 na Nicki. Kutokana na hali hiyo amekuwa akijifungia ndani usiku na mchana akivuta bangi na amezungumza wazi kuhusu kutaka kujitoa uhai wake.

Safaree anawaambia washkaji zake kuwa hawezi kumpata tena Nicki kwasababu ana uhusiano na Meek Mill. Anasema hiyo ni adhabu kwake kwakuwa anaamini Meek Mill ndiye aliyemharibia kwa Nicki kwa kwa madai ya uongo kuwa alimsaliti.

Marafiki zake wamesema wanahofia kuwa hivyo si vitisho vya kupuuzia.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents