Burudani

Evance Bukuku wa Vuvuzela aeleza sababu za kumchukua mdogo wake muimbaji Enika kwenye comedy

Enika ni msanii wa kike ambaye nyota yake ilianza kuonekana mwaka 2004 alipotoa wimbo wake wa ‘Baridi Kama Hii’, ambao ulishika chati mbalimbali za muziki Bongo. Enika ambaye jina lake kamili ni Atuganile A Bukuku ni dada wa aliyekuwa producer wa G Records na baadae G2, marehemu Roy Bukuku, pamoja na Evance Bukuku wa Vuvuzela Comedy.

Enika

Producer Roy ndiye aliyekuwa mwanga wa career ya muziki ya Enika, pia ndiye aliyeproduce single yake ya ‘Baridi Kama Hii’, lakini toka afariki 2008, Enika hakuendelea tena kufanya muziki na badala yake hivi sasa anafanya comedy na kaka yake Evance japo ni wengi ambao wamekuwa wakitamani kumsikia akiendeleza kipaji chake.

Evance mkasi

Hivi karibuni Evance Bukuku alihojiwa na Salama Jabir kupitia kipindi cha Mkasi na kuulizwa swali kuhusu Enika kuingia kwenye comedy na kuacha muziki.

Hili ndio lilikuwa swali la Salama kwa Evance:

“Enika ni msanii mzuri sana, miaka ya nyuma alihit sana, na mtu aliyekuwa anamtengenezea muziki mzuri alikuwa ni kaka yake marehemu…and then mwenyeji Mungu akamchukua. Career ya muziki ya Enika kama ikapotea hivi na mpaka sasa hivi tunavyozungumza Enika hafanyi muziki anafanya comedy pamoja na wewe…Ulimchukua Enika kwenye kundi lako kufanya naye kazi kwasababu ni mcheshi kweli, ama ulimchukua kwaajili ya kumwondoa pengine kimawazo kumwondoa sehemu moja umpeleke sehemu nyingine”

Na hiki ndicho alichojibu Evance:

“Enika is very talented…Kumchukua pale nafahamu uwezo wake na uwezo wake ndo huo unaoonekana, herself as a comedian, not like she is funny, lakini comedy inaundwa, kama kipindi hiki kinaundwa , so if you write nice material …performed the way she performs it’s a product”.

http://youtu.be/ohqsT865IG8

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents