Videos

Video: Esther Wasira- ‘Viongozi Waache Kutoa Cheap Answers’

Mwanajamii na mwanaharakati Esther Wasira ameongea na bongo5.com na kusema kwa sasa hatofanya tena muziki wa Bongo Flava kibiashara na badala yake atajikita kwenye Siasa ili aendelee na harakati za kuwatetea Watanzania ili wapate Maisha bora yenye neema.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ambayo utapata fursa ya kuyaangalia hapa chini, Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya yeye kuchagua kuchukua uanachama wa Chadema hata kama ukoo wake upo CCM, ni baada ya kufanya uchunguzi na kugundua kuwa Chama cha Chadema kinaonekana kina nia njema na ya dhati ya kuwakomboa na kuwaletea mabadiliko watanzania.

Kwa kifupi, katika mahojiano hayo ameongelea mambo mengi yanayohusu mustakabali wa watanzania, kama Rushwa, Uwajibikaji, Ufisadi, uongozi thabiti, uzalendo, na pia aligusia kama atafanya nyimbo basi ni ya kwaya.

Angalia mahojiano hayo hapa chini kufahamu kwa undani, ameyaongeleaje masuala hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents