Burudani

Eric Omondi aipa shavu ‘Muziki’ ya Darassa kwenye comedy yake ya Adam na Eva

Eric Omondi anapojitayarisha kuja na LIVE TV show yake ya comedy nchini Tanzania, tayari moyo wake ulilowekwa na kulowa chepechepe na upendo aliopewa na bado anaupata kutoka kwa mashabiki wa Bongo.

Ni baada ya kukutayarishia segments za comedy kama vile ”How to be like Diamond” ambayo iliwachangamsha mashabiki wa Diamond kote Afrika kwa kuiga vipengele fulani kwenye maisha binafsi ya staa Platnumz. Na nyingine ”How to be like Magufuli” ambayo aliiga nakuelezea hulka za Mheshimiwa rais wa sasa wa Tanzania Dkt John Magufuli, vipande hivi vya video fupi za comedy kutoka kwa Eric Omondi unaweza vipata kwenye channel yake ya YouTube.

Omondi ambaye kwa ajili ya Valantine ama siku ya wapendanao, alituletea segment mpya kwa jina Adam and Eve, inayotamba na tayari ndani ya siku sita zilizopita imefikisha zaidi ya views 144k, kwenye channel yake ya YouTube, ametumia vipande vya muziki kutoka kundi la muziki la hapa nchini Kenya la Heart The Band ”Nikikutazama” na kipande kidogo kutoka kwa wimbo wa rapper mkali anayependwa kwa hivi sasa Darassa kwenye wimbo wake ‘Muziki.’

Katika sehemu moja kwenye segment hii kutoka kwa Eric Omondi na mrembo wake Chantal Graziola, ambaye pia ndiye mchumba wake Eric mwenye asili ya kikenya na kitaliano, Chantal ambaye aliiga kama Eve, anaonekana akimuamsha Eric (Adam) ili aule tunda alilopewa na nyoka kulingana na vitabu vitakatifu. Na baada ya Eric kuamka, baadala ya kumpa tunda kama wengi walivyotarajia Chantal Graziola anampa Eric ear-phone asikilize favourite song yake, ambayo ni ngoma Muziki ya Darassa.

Darassa anakuwa staa wa pili kutoka Bongo baada ya Diamond kuugusa moya wa Eric ambaye hajaweza kuficha hilo kwa kuamua kuutumia wimbo wake Muziki…Pata uhondo zaidi kwenye kipande hiki cha comedy hapa chini upate uhakikisho zaidi.

Makala ya: Changez Ndzai ( Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents