Habari

Edward Lowassa akana kumiliki ukurasa wowote wa mitandao ya kijamii

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa amekanusha kumiliki kurasa za kijamii Facebook,Twitter, Instagram.

LOWASSA

Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi yake,inasena:Kumekuwa na kurasa(accounts) mbalimbali zenye jina la Mh Edward Lowassa katika mitandao ya kijamii Kama vile facebook,Twitter, Instagram nk.Zinaonekana mmiliki wake ni Mh Edward Lowassa.

Ukweli ni kwamba hizo zote hazimilikiwi na Mh Lowassa. Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo hazihusiani kwa namna yoyote na Mh Lowassa.

Hata hivyo Mh Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.

Imetolewa na
Ofisi ya Mh Edward Ngoyai Lowassa (MB)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents