Bongo Movie

DVD ‘feki’ za filamu zenye thamani ya Tsh bilioni 4 zakamatwa kwa kipindi cha miezi 3

Opereshini za serikali za kuwakamata wauzaji wa DVD ‘feki’ za filamu zinazoendeshwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali kwa kipindi cha miezi mitatu zimefanikisha kukatwa kwa mzigo wa DVD ‘feki’ wenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni 4.

Akiongea na Bongo5 wiki hii Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo, amesema operesheni hizo zitaendeshwa mara kwa mara ili kupambana na wimbi la DVD hizo feki za filamu ambazo zinawanyima wasanii kipato pamoja na serikali.

“Mh Waziri Nape Nnauye waziri wetu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amekuwa mstari wa mbele katika kupigania kazi za wasanii, na moja mifano aliyoonyesha yeye mwenyewe ni kwenda mtaani na kukamata kazi mbalimbali, na mwezi wa pili tarehe 18 tulikamata kazi zenye dhamani zaidi ya biloni 4 na ninaamini tukiendelea hivi itakuwa funzo kwa hao wanaofanya biashara hiyo,” alisema Bi.Joyce Fissoo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents