Dunga amerudi kwao?

Dunga amerudi kwao?
Inasemekana kuwa Ambros Nkwabi aka Dunga ameamua kurudi nchini kwao Kenya baada ya kupiga mzigo kwa miaka mitatu mfululizo na kuproduce hits kibao ndani ya Bongo.

Maneno mitaani ni kwamba Dunga ameamua kurudi kwao baada ya Work Permit yake kuisha muda na kushindwa kuongeza muda huo.

Ni kweli kwamba Dunga ni producer mkali sana, zaidi kuna watu wanaosema kwamba alileta tishio kubwa kwa wapinzani wake kibiashara na kuteka muziki wa Bongo Flava kitu ambacho hakikuenda sawa na baadhi ya watu waliyokuwa wakimpinga hadi kufikia hatua ya kujaribu kutoa rushwa ili work permit yake isiongezwe muda.

Kwa sasa yupo mjini Nairobi pamoja na kaka yake Shaky na wameshaanza kuproduce tracks kwa ajili ya wasanii wa huko.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents