Burudani

Dully Sykes: Nikipata upenyo wa kuongea na T.I. ntaomba collabo

Prince Dully Sykes amesema yeye ni miongoni mwa wasanii wanaousubiria kwa hamu ujio wa rapper T.I. kutoka Marekani.

Dully Sykes

Dully aliiambia Bongo5 kuwa kufika kwa rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Clifford Joseph Harris nchini ni jambo kubwa na historia nzuri katika muziki wa Tanzania.

“Kwangu mimi ujio wa T.I, bongo ujue tunaandika historia mpya katika muziki. T.I. ni msanii mkubwa sana na sasa hivi yupo hot na dunia nzima inamwangalia, kwahiyo kwetu sisi ujio wake ni mafanikio katika muziki wetu. Kama nikipata nafasi ya kuongea naye kikubwa ni kolabo tu, nikifanya naye kolabo basi,” alisema Dully.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents