Burudani

Dully Sykes: Mbona wasanii wa US wanaimba matusi hamsemi? Au hamwelewi Kiingereza!

Dully Sykes amesema haelewi kwanini watu wanamshangaa baada ya kutoa wimbo wenye matusi wakati nyimbo za wasanii wa Marekani zimejaa uchafu mwingi.

Dully-Sykes-1

Wimbo huo unaitwa ‘That’s the Way’ na amemshirikisha Maunda Zorro.

“Kwani kuna nyimbo ngapi za matusi zinatoka Marekani na watu wanaziangalia,” amehoji Dully. “Mbona kuna movie zinaangaliwa na watu hawalalamiki? Hii ni kama movie ambayo ndani yake kuna mambo ambayo watoto hawaruhurusiwi kuiangalia, inabidi watoto wenye umri chini ya miaka 18 wasiusikilize.”

Dully anadai kuwa wimbo huo umevuja tu.

“Huu wimbo kuna mtu ameuiba na kuutoa ili kunifanyia mimi uhuni, najutia kwa nini umepotea vipi sijui! Lakini mbona kuna nyimbo nyingi zipo hivi au kwa sababu watu hawajui Kiingereza? Kuna wimbo kama Anaconda (Nicki Minaj) mbona unapigwa na bado una matusi!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents