Burudani

Dully Sykes kuja na wimbo uitwao ‘Banza Stone’

Dully Sykes anatarajia kuja na wimbo tofauti.

11015505_622198391250438_1731865975_n

Muimbaji huyo mkongwe ameiambia Bongo5 kuwa anatarajia kuja na wimbo uitwao ‘Banza Stone’.

“Nimefanya huo wimbo ili kukubali kazi yake na kumkubali kama mwanamuziki ambaye alistahili tuzo kubwa sana sababu yeye ni kati ya wale wanamuziki wakubwa waliofanya muziki wa dansi kupendwa Tanzania,” amesema Dully.

“Katika wasanii waliokuja wakatikisa kipindi hicho mimi naanza muziki ama natafuta njia ya kutoka kwakuwa nilikuwa nimeshaanza muziki ila nilikuwa natafuta njia ya kutoka lakini mtu kama Banza Stone nilikuwa namsikiliza, namuangalia yeye,” ameongeza.

Dully amesema wimbo huo upo kwenye mahadhi ya Rhumba.

Banzo Stone ni miongoni mwa waimbaji wa muziki wa dansi wanaoheshimika zaidi nchini na amewahi kuimba na bendi nyimbi kubwa ikiwemo Twanga Pepeta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents