Burudani

Dully Sykes kuachia wimbo mpya uitwao Yono, atumia chorus ya wimbo wa Jose Chameleone

By  | 

Msanii mkongwe wa muziki nchini, Prince Dully Sykes anajipanga kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Yono’ baada ya kufanya vizuri na wimbo Inde ambao alimshirikisha Harmonize wa WCB.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa kwenye wimbo huo ametumia chorus ya wimbo wa zamani wa Jose Chameleone ambao ulikuwa kwenye albamu ya muimbaji huyo iliyotoka mwaka 2003.

“Mungu akipenda kesho naachia mkwaju wangu mpya wimbo unaitwa Yono, chorus ya wimbo nilipewa na Jose Chameleone toka mwaka 2003 baada ya kuipenda nikamwambia akaniruhusu kuitumia,” alisema Dully.

Aliongeza, Kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwa sababu kazi ni nzuri, pia itatoka pamoja na video yake kwa sababu kila kitu kipo tayari yaani tumejipanga,”

Muimbaji huyo alisema kazi hiyo imeandaliwa katika studio yake mwanzo mwisho.

Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumsupport katika muziki wake kama walivyomsupport kwenye wimbo wake uliyopita akiwa na Harmonize.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments